Ijumaa, 2 Mei 2014

WATU 19, WAMEUWA BAADA YA KUTOKEA MLIPUKO KATIKA MJI KUU WA NIGERIA, ABUJA.

Baadhi ya watu waliojeruhiwa katika mlipuko huo.
Mkurugenzi wa idara ya kushughulikia mikasa na hali ya dharura- FEMA- Abbas G Idriss, alisema watu 60 walijeruhiwa lakini sita kati yao wametibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani, ambapo magari sita yameharibiwa katika mlipuko huo.

Mlipuko huo ulitokea katika eneo la Nyanya, karibu na kituo cha basi ambako zaidi ya watu 70 waliuwawa katika shambulizi la tarehe14 mwezi Aprili.

Waandishi wanasema kuwa mlipuko huo umesababishwa na bomu lililotegwa ndani ya gari. Mmoja wa walioshuhudia kisa hicho amesema aliona miili 20 ya watu waliouwawa.

Hakuna kundi lililodai kuhusika katika shambulizi hilo lakini kundi la wanamgambo wa kiislamu la Boko Haram limewahi kutekeleza mashambulizi kama hayo mjini Abuja

Mengi ya mashambulizi ya Boko Haram yamekuwa yakitokea katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria, lakini shambulizi la bomu la Aprili 14, lilizua hofu kwamba huenda wanamgambo hao wameanza kupanua maeneo wanayoendeleza harakati zao.

Hakuna maoni: