Jumanne, 6 Mei 2014

CAMERA YA SUNBIRD MTAANI LEO.

KIJANA akiwandaa samaki katika soko la Kimataifa la feri wakiandaa samaki kwa ajili ya kuuzwa, hata hivyo baadhi ya wananchi wamelalamikia kuhusu eneo hilo kukithiri kwa uchafu sokoni hapo kunakopelekea kuhatarisha afya za wateja.

MITA ya umeme ikiwa imeachwa wazi katika eneo la Mnazimoja, Dar es alaam, jana, huku mvua zikiendelea kunyesha kunakopelekea kuhatarisha usalama wa wananchi wanaopita katika eneo hilo.

LICHA ya kufanyiwa matengenezo kwa kuziba sehemu zilizochimbika, barabara ya uhuru imekuwa ikijaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam. Tatizo la kuja kwa maji kwa barabara hiyo ni kukosekana kwa mitaro ya maji ya mvua au mitaro kuziba.


Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

Posted by whom?