Jumatano, 21 Mei 2014

SHEREHE YA UFUNGUZI MAADHIMISHO YA SIKU YA UANUAI YA UTAMADUNI NA UHURU WA AFRIKA KATIKA VIWANJA VYA MNAZIMOJA, DAR ES SALAAM, LEO.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mikangara azindua maonyesho ya siki ya Utamaduni na Utamaduni, katika viwanja vya Mnazimoja, Dar es Salaam.


Kikundi cha ngoma asili kutoka Mkoani Dodoma kikitoa burudani viwanjani hapo, leo.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Magomeni wakionyesha umahiri wa sanaa ya uchoraji.

Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Bao Tanzania (SHIMBATA) Monday Likwepa akimfundisha kucheza mchezo wa bao Magreth Mapunda, jana wakati maadhimisho hayo.


Mchezo wa kukuna nazi ambao asili yake ni Mikoa ya Pwani, Bi. Sophia akionyesha umahiri wa kukuna nazi wakati wa maonyesho hayo.
Ngoma ya Solo kutoka Tanga moja tamaduni zinazovutia kuangalia ambapo ilitia fora kwa watizamaji wake kupata burudani ya kutosha.

Ngoma ya mganda kutoka kwa wanyasa ikitoa burudani kwa watu waliofika katika uzinduzi hio ulioambatana na maonyesho.


Dk. Fenella Mukangara akicheza ngoma ya wanyasa ambayo ilikuwa kivutio kikubwa kwa watizamaji.


Mchezo wa bao ulikuwa kivutio kikubwa kwa wananchi waliofika katika viwanja hivyo kushudia mambo mbalimbali ya utamaduni.


Mpanda baiskeri naye hakuwa nyuma kuonyesha namna umahiri wake wa kupanda baiskeri.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akiwa katika uzinduzi wa siku ya uanuai ya utamaduni na uhuru wa Afrika, amabapo alitembelea mabanda na kujionea tamaduni mbalimbali, jana.

Hakuna maoni: