Pia, imetakiwa kutenga bajeti maalum kwa ajili ya kupambana na saratani ya ngozi kwa watu wenye ualbino kwa kutoa kinga, tiba na mafunzo.
Hayo yalisemwa na Mjumbe wa Chama cha Albino Tanzania Husein Kibindu wakati akisoma risala Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Seif Rashid, kwenye maadhimisho ya siku ya Ualbino, katika viwanja vya Mnazimoja, Dar es Salaam, jana.
Kibindu alisema kuanzia mwaka huu kumekuwa na taarifa za matishio kwa akina mama na watoto wenye ualbino katika mikoa ya kanda ya ziwa, ambapo sababu kubwa ikielezwa kuwa ni imani potofu za kishrikina.
Alisema imani potofu kwa upande wa mikoa hiyo imekuwa iko juu, ambapo kuna mikasa ya mauaji ya watu wenye ualbina na wasiokuwa ualbino, wakiwemo wanawake na watoto.
Aidha, Kibindu alisema vitendo vya mauaji na uakataji wa viungo kwa watu wenye ualbino unapelekea watu na familia zao kupata madhara ya kisaikolojia na kwasababishia umaskini kutokana na kupoteza viungo vya miili yao.
WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Jeshi la Wokovu Kurasini jijini, Dar es Salaam, wakiwa katika viwanja vya Mnazimoja, wakati wa maadhimisho hayo, ambayo kitaifa yalifanyika jijini Dar es Salaam. |
KIKUNDI cha sanaa cha Ualbino wakitoa burudani mbele ya wananchi waliofika katika siku hiyo ya maadhimisho. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni