Karibu katika ulimwengu wa habari.Hapa utapata habari mbalimbali kukuelimisha, burudisha na kuwa wa kwanza kabisa kujua mambo mbalimbali.
Jumanne, 13 Mei 2014
MISRI YATOA VIFAA TIBA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI KUBORESHA HALI YA AFYA NCHINI.
Serikali Misri imepatia msaada wa vifaa tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), kwa ajili ya kuboresha huduma za Urolojia hospitalini hapo.
Vifaa hivyo vyenye thamani ya sh. milioni 405,000,000, vilitolewa na Balozi wa Misri Nchini Hossam Mharam ambapo alimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo Dk. Marina Njelekela.
Huduma za Urolojia katika hospitali ya Taifa Muhimbili zilianzishwa mwaka 2008, chini ya Idara ya upasuaji kwa lengo kuboresha huduma kwa wananchi.
Kitengo cha Urolojia hutoa huduma kwa wagonjwa wa uvimbe wa tezi dume (BPH), kuziba kwa njia ya mkojo kutokana na kovu (Urethra Stricture), saratani ya kibofu (Bladder Cancer), saratani ya tezi dume (Prostate Cancer) na mawe kwenye kibofu (Kidney Stone).
Akishikuru kwa niaba ya serikali, Mkurugenzi wa (MNH), Dk. Marina alisema vifaa tiba hivyo vimekuja wakati muafaka ambapo serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inatekeleza mkakati wake wa kuboresha huduma za afya
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni