Oscar Pistorius anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp nchini Afrika Kusini. |
Jopo la utetezi katika kesi ya mauaji inayomkabili mwanariadha waAfrika Kusini, Oscar Pistorius limeitisha mashahidi zaidi, wakitaka kuthibitisha kuwa mwanariadha huyo alimuua mpenzi wake Reeva Steenkamp bila kukusudia.
Majirani wa Pistorius walisema siku ya Jumanne, walisikia mtu akilia kwa nguvu usiku wa mauaji hayo.
Jumatatu watu wengine wawili ambao walikuwa wa kwanza kufika eneo la tukio walielezea juhudi alizokuwa akifanya kuokoa maisha ya Steenkamp.
Mwanariadha huyo anatuhumiwa kumuua mpenzi wake huyo Steenkamp siku ya Valentine, mwaka jana.
Hata hivyo katika kesi huyo, Pistorius amekana tuhuma za kumuua makusudi mpenzi wake na alisema alimpiga risasi kupitia mlango wa chooni akiwa ametaharuki, akidhani mtu aliyekuwa anamshambulia ni mwizi aliyeingia nyumbani mwake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni