Jumatatu, 5 Mei 2014

AWAMU YA KWANZA WA MRADI WA MABASI YAENDAYO HARAKA, JIJINI DAR ER SALAAM, KUKAMILIKA MWAKA HUU.


OFISA Uhusiano wa Mradi wa Mabasi yaendayo haraka(DART), William Gatambi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi huo ambao utasaidia kupunguza foreni katikati ya jiji la Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Uendashaji wa mradi huo Peter Munuo na Kulia ni Ofisa Habari wa MAELEZO, Frank Mvungi.
MRADI wa mabasi yaendayo kasi (DART) unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu ambapo kwa awamu ya kwanza mabasi makubwa 20 na madogo 10 yatakuwa majaribio.

Akizungumza, jijini Dar es Salaam, Meneja uendeshaji wa DART, Peter Munuo aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maendeleo mradi huo.

Munuo alisema wanatarajia kuanza kutoa huduma ya mpito Desemba mwaka huu ambapo mwakani huduma kamuli itaanza rasmi.

Alisema kwa kipindi hiki cha huduma mpito mabasi ya Meneja huyo alisema hayo mabasi ya majaribio yana uwezo wa kubeba abiria ya 140 hadi 160 hadi watakapoanza kutoa huduma kamili ifikapo mwaka 2015, hivyo yatasaidia kupunguza msongamano wa watu unaosababishwa na shida ya usafiri.

Alisema kwa mujibu wa tafiti ambazo wamezifanya ndani na nje ya nchi, imebainika kuwa mfumo wa mabasi yaendayo kasi ndiyo unaoweza kupunguza msongamano wa watu na tatizo la usafiri.

Hakuna maoni: