Alhamisi, 1 Mei 2014

MWANASIASA MAARUFU WA CHAMA CHA SINN FEIN, GERRY ADAMS, AKAMATWA KASKAZINI IRELAND.


JESHI la Polisi nchini Kazkazini Ireland wamemkamata mwanasiasa mashuhuri wa chama

cha Sinn Fein, Gerry Adams kwa kuhusishwa na mauaji yaliyotokea zaidi ya miaka 40 iliyopita.

Adams anahojiwa kuhusu mauaji ya Jean McConville ambaye alitekwanyara na kundi la waasi

la IRA mnamo mwaka 1972 na kisha akapatikana amepigwa risasi na kuuawa .

Kiongozi huyo amekanusha kuhusika kivyovyote vile akisema kuwa alijipeleka binafsi kuzungumza na

polisi ilikujaribu kusuluhisha madai hayo yaliyomwandama kwa miaka mingi mno .

Adams anakanusha kuhusika kwa vyovyote vile na utekaji nyara wala mauaji yake bi Mc Conville

ambaye alikuwa mama wa watoto 10 .Madai hayo yanafwatia mahojiano mjini Belfast

mwaka wa 2001-2006 baina ya chuo kikuu cha Boston Marekani na wakereketwa wa vita hivyo

vilivyonuiwa kuikomboa Ireland kutoka kwenye minyororo ya ukoloni.

Mahojiano hayo yalifanywa kwa misingi kuwa yangewekwa siri hadi baada ya vifo vya wahusika

wakuu, lakini baada ya kesi za kutaka kutambulika wahusika na wahasiriwa waliotoweka wakati wa

vita hivyochuo hicho kililazimishwa kutoa sehemu ya mahojiano kwa serikali ya Ireland.

Mmoja kati ya watu 16 waliosemekana kutoweka ni Mc Conville, hata hivyo mjane huyo alilaumiwa na

IRA kuwa mpelelezi wa polisi lakini baada ya ufafanuzi wa polisi yapata mwaka wa 1999, ambapo

McConville ilibainika hakuwa.Kundi hilo la IRA lilikiri kutekeleza mauaji yake bi

McConville mwaka wa 1999 lakini mwili wake ulipatikana mwaka wa 2003 ukiwa umetupwa

kwenye ufukwe wa bahari.IRA inashtumiwa kwa kampeini na mauaji

yaliyotikisa Ireland kaskazini kwa takriban miaka 30.

Chanzo: BBC SWAHILI.

Hakuna maoni: