Wagombea wanaochuana katika nafasi ya Urais nchini Mlawi. |
Raia wa Malawi leo wanafanya uchaguzi mkuu ambapo wagombea 11, wanawania kiti cha urais dhidi ya rais Joyce Banda.
Joyce ambaye aliingia madarakani miaka miwili iliyopita baada ya kifo cha rais Bingu wa Mutharika - alipendwa na umma wa Malawi, lakini sifa zake zilipungua kufuatia kashfa kama ya Cashgate.
Aidha, Joyce anakanusha kuhusika kwa namna yoyote ile na kashfa hiyo.
Hata hivyo wachambuzi wengi wa masuala ya siasa nchini Malawi wanabashiri kuwa yeye ndiye anayependwa na wengi hususan katika maeneo ya vijijini .
Uchaguzi huo unatarajiwa kuwa na mchuano mkali kuwahi kushuhudiwa katika taifa hilo la Malawi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni