Jumapili, 11 Mei 2014

WAKONGWE WA MADRID KUJA NCHINI MWEZI AGOST MWAKA HUU.






Real Madrid ya Hispania inatarajia kuja nchini mwezi Agost, mwaka huu kwa ajili ya mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania.

Jana, Mkurugenzi wa Makampuni ya TSN, Farough Baghoza na Nahodha wa klabu hiyo Ruben De la Red, walisaini mkataba wa ujio wa timu hiyo inawahusisha wachezaji waliowahi kuwika duniani na klabu hiyo.

Jumla ya wachezaji 25, wakongwe ambao waliowahi kuitumikia klabu hiyo kubwa Dunia wataambatana na wachezaji ambao wanaitumikia klabu hiyo hadi sasa.

Azungumzia ujio wa timu hiyo Mwakilishi wa TSN, Dennis Seboa alisema ujio wa wachezaji hao wakongwe watasaidia kuinua hali ya mchezo wa soka hapa nchini.

Sebo alisema wakongwe hao watapata nafasi ya kutembelea mbuga za wanyama kwa ajili kuitangaza utalii wa Tanzania, nchini Hispania ambapo aliyekuwa nahodha wa timu hiyo Fernando Hierro atapanda mlima Kilimanjaro ambapo televisheni ya Real madrid itaonyesha tukio hilo maja kwa moja.

Naye Nahodha wa timu hiyo ya wakongwe Ruben De la Red alisema wanatambua kuwa nchi ya Tanzania ina mashabiki wengi wanaopenda soka ambapo anaamini mechi hiyo itakuwa kali.

Aidha, alitoa angalizo kwa timu ya Tanzania kuwa wao bado wanafanya mazoezi kila siku na wako vizuri kiuchezaji hivyo timu ya vijana ya watanzania wafanye mazoezi ya kutosha.









Nahodha wa klabu ya wakongwe wa Real Madrid Ruben de la Red akizungumza na waandishi wa habari jana, Dar es Salaam, baada ya kutiliana saini na Makampuni ya TSN. Kushoto ni Mchezaji wa Klabu hiyo aliyewahi kuwika Rayo Gacial.


Rais wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF), Jamali Malinzi akikabiziwa jezi ya Madrid na Nahodha wa Ruben de la Red 
Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa akikabidhiwa jezi ya madrid.

Hakuna maoni: