|
Victor Nealon |
Aliyefungwa jela kwa miaka 17, kimakosa ameombwa radhi nchini Uingereza.
Victor Nealon (53) alihukumiwa jela baada ya mahakama kumkuta na hatia ya kosa la kujaribu kumbaka mwanamke, ingawa tume ya kuchunguza kesi za watu waliofungwa jela kimakosa imemuomba radhi.
Nealon, alihukumiwa kwa kosa la kumshambulia mwanamke nje ya ukumbi wa densi mwaka 1996.
Ambapo aliomba tume ya kuchunguza kesi za wafungwa waliohukumiwa kimakosa kuchunguza kesi yake ingawa alipuuzwa mara mbili.
Tume hiyo sasa imesema ilipaswa kuchunguza kesi yake kwa umaakini ingawa hilo halikufanyika.
Mwenyekiti wa tume hiyo Richard Foster alisema kuwa anajuta kwa sababu kuna jambo fulani katika kesi hiyo ambalo hatukulichunguza vyema, tunamuomba radhi mwathiriwa.
Nealon, ambaye alikana madai ya njama ya kumbaka mwanamke huyo, alikamatwa baada ya madai kuwa mwanamume huyo alimdhulumu kimapenzi akiwa anarejea nyumbani kutoka klabuni katika mtaa wa Redditch.
Mtuhumiwa alifungwa jela baada ya mahakama kumpata na hatia na kumhukumu maisha jela.
Hata hivyo, Mawakili wake ndio waliochunguza ushahidi huo na kupata chembechembe za DNA ambazo sio zake bali za mtu asiyejulikana na kukosoa polisi kwa kuficha ushahidi huo.
"Ningekuwa nimeondoka jela miaka 10 au12 iliyopita lakini kutokana na kosa la tume kukosa kuchunguza kesi yangu, ilinibidi kuhudumia kifungo
kwa kosa ambalo sikufanya'', alisema Nealon.