Jumanne, 22 Julai 2014

WATU WANANE WANASHIKILIWA KUTOKANA NA TUKIO LA KUKUTWA KWA VIUNGO VYA BINADAMU, ENEO LA BUNJU, DAR ES SALAAM.

KAMISHNA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akielezea kuhusu tukio la kutupwa viungo vya binadam katika bonde la Mbweni Mpiji, eneo la Bunju, Dar es Salaam. 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dara es Salaam, limebaini kuwa viungo vya binadamu vilivyokutwa eneo la bonde la Mbweni Mpiji, kata ya Bunju, Dar es Salaam, kwa mara ya mwisho vilikuwa katika maabara ya Chuo Kikuu cha Madaktari (IMTU).
Polisi linawashikilia watu wanane wakiwemo madaktari wa IMTU kwa ajili mahojiano kwani inasadikiwa kuhusika na kuweko kwa viuongo hivyo.
 Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar e Salaam, Suleiman Kova alisema chuo hicho hufanya mafunzo ya udaktari kwa vitendo.
Alisema Jeshi hilo limeunda jopo maalumu la wapelelezi kwa ajili ya kuchunguza tukio la kuweko kwa vifaa hivyo ambapo limewashikilisha Mkuu wa Upelelezi wa Kanda hiyo ACP, Japhari Mohamed kwa kusaidiana na Daktari wa Jeshi la Polisi anayehusika na masuala ya uchunguzi wa miili ya binadamu na madaktari wengine kutoka katika Hoaspitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Tukio hilo lilitokea juzi katika eneo la Bunju, ambapo viungo vya binadamu vilikutwa katika mifuko ya plastic 85, ambapo ndani yake kulikuwa na Vichwa, Miguu, Mikono, moyo mapafu, vifua na mifupa mbalimbali ikiwa vimekaushwa na havikuwa na uvundo.
Pia, katika eneo hilo kulikutwa vifaa vya kufanyia operesheni ikiwemo nguo malum (Apron) 20, mipira ya kuva mikononi pamoja na karatasi ya maswali na majibu.

Hakuna maoni: