Kaimu Mkurugenzi wa Benki hiyo, Said Said, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ, wakati wa hafla hiyo futari alisema amana ya benki hiyo imekuwa ikiongezeka kutoka asilimia 30 hadi 40, ambayo ni kubwa ukilinganisha na soko la mabenki.
Said alisema PBZ, iko katika hatua za mwisho kufungua matawi mengine manne, yatakayoendeshwa kwa mfumo huo, pamoja kuborsha huduma kwa wateja wao.
Aidha, Said alisema benki hiyo imerahisisha huduma kwa wateja kwani wanaweza kutumia mtandao wa intanet na simu ya mkononi pamoja na kusafirisha fedha kutoka nje ya nchi kwa wateja wanaoishi nje ya nchi.
Wafanyakazi na wateja wa benki hiyo wakiwa katika hafla hiyo. |
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymound Mushi akiwa katika futari uliyoandaliwa na PBZ. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni