Mwenyeki wa mpya wa shina la Wakeleketwa CCM, Pamba road, Sharik Choughule amesema atahakikisha chama hicho kinashinda chaguzi za serikali za mtaa na uchaguzi wa mkuu wa 2015.
Choughule alisema hayo juzi baada ya kuchaguliwa mwenyekiti mpya wa shina hilo katika uchaguzi uliofanyka katika ukumbi wa Karemjee, Dar es Salaam.
Alisema kazi iliko mbele yake ni kuhakikisha kukiletea chama maendeleo pamoja kuendeleza umoja uliko ndani ya shina hilo liloko katikati ya jiji la Dar es Salaam, maeneo ya Posta.
"Siwezi kuongea maneno mengi ila vitendo vyangu vitaonekana kwa kuiletea CCM, maendeleo na tawi shina letu, suala la msingi ni kushirikiana na wanachama wenzangu, kwani nina uzowefu wa uongozi kutokana na kuwa Kamanda wa Vijana Kata ya Kivukoni", alisema Choughule.
|
Sharik akwa na mpinzani wake kabla ya uchaguzi ndani ya ukumbi wa Karemjee, Dar es Salaam. |
|
Wagombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Shina la CCM, Pamba road wakiwa mbele ya wapiga kura kabla ya kila mmoja kuomba kura. |
|
Mwenyekiti mpya wa Shina la Pamba Road Sharik Choughule akiwa mwenye furaha baada ya kumalizika kwa kuhesabiwa kura. |
|
Wanachama wakipiga kura katika uchaguzi huo. |
|
Akitangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa tawi hilo. |
|
Akipongezwa na mpinzani wake aliyechuana naye katika uchaguzi uliomuweka madarakani Shariki, ambaye pia ni Kamanda wa Vijana, CCM, Kata ya Kivukoni. |
|
Akikabidhiwa kiti rasmi na mwenyekiti wa uchaguzi, kulia ni Katibu wa shina. |
|
Mwenyekiti mpya akinyanyuliwa juu juu |
|
Akisalimia wanachama akiwa makao Makuu ya Shina hilo la Pamba road, maeneo ya Posta, Dar es Salaam. |
|
Mgombea aliyejitoa katika hatua za mwisho akipiga kura yake. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni