Mkutani uliofanyika jijini Dar es Salaam, Viongozi wa vyama vya walichangia mjadala kuhusu namna ya kuboresha daftari hili lilotarajiwa kuanza mwezi septemba mwaka huu, nchi nzima.
Katika mkutano huo vyama vya upinzani viliwakilishwa na viongozi wao akiweo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Wilbrod Slaa, Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu. Vyama vingine vilivyokuwa katika mkutano huo ni pamoja na Sauti ya Umma (SAU), CCK.
Mfumo mpya unaojulikana Biomettric Vote Registration (BVR), uliotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ambayo mwenyekiti wake ni Jaji Mstaafu Damian Lubuva.
|
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana akizungumza na vyombo vya habari wakati wa mkutano huo. |
|
Mwenyekiti wa CUF, akielezea jambo kwa waandishi wa habari kuhusu mfumo huo mpya wa kuboresha daftari hilo. |
|
Kushoto ni Tundu Lissu, Slaa na Lipumba wakiteta jambo kuhusu mfumo huo mpya wa kuliboresha daftari hilo la wapiga kura utakaoanza Septemba mwaka huu. |
|
Dk. Slaa akitoa ufafanuzi kuhusu mfumo huo kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Lubuva. |
|
Kinana akifuatilia kwa makini maakaratasi yenye taarifa kuhusu mkutano huo ambao ulikuwa unaelekeza namna ya mfumo huo wa BIOMATRIC VOTE REGISTRATION unaweza kufanyakazi. |
|
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini. |
|
Kinana akizungumza jambo na Mwenyekiti wa UDP, John Cheo kwenye mkutano wa viongozi wa vyama vya siasa kuhusu kujadili uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ulioandaliwa na Tume ya Taifa Uchaguzi(NEC), Dar es Salaam.
|
|
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana akisalimiana na Katibu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa. |
|
Mashine maalum itakayotumika kutengenezea vitambulisho vya kupigia kura, inajulikana BIOMATRIC VOTE REGISTRATION (BVR).
|
|
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (Mtaafu), Damian Lubuva akieleza kuhusu uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura kwa kutumia mfumo mpya Biometric Vote Regstration (BVR).
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni