Rais Mteule wa Klabu hiyo, Dk. Hussein Hassan, alizema lengo la msaada huo ni kuwajali watu wenye matatizo ili nao wajione sehemu ya jamii.
Alisema msaada huo ni sehemu mojawapo ya shughuli za za klabu hiyo katika kusaidia jamii kwa kuwa saidia miradi mbalimbali ya kijamii.
"Tumekuwa tukisaidia watu wenye ulemavu, watoto wa mitaani, wajane, kugawa miwani kwa wenye matatizo ya macho, kuanzisha miradi ya maendeleo pamoja kufanya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali", alisema.
Aidha, alisema klabu hiyo imeambatana na wajumbe wake wakiwemo wawili kutoka nchini marekani ambao wako nchini kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na klabu hiyo.
Pia, Hussan alisema wanatarajia kupokea msaada wa jozi 400 ya miwani ya macho kutoka kwa wajumbe hao, ambapo msaada huo utatolewa kwa jamii.
Chakula kikipakuliwa kwa ajili kusambaza kwa wagonjwa waliorazwa hospitalini hapo. |
Rais wa Lions Club, Dk. Hussein Hassan akiwaongoza wanachama wenzake katika kupakua chakula hicho ambacho kiligawiwa kwa wagonjwa 300. |
Mgonjwa akipewa chakula kutoka kwa mwanachama wa klabu ya Lions klabu ya Aman hospitalini hapo. |
Kulia ni Director wa Klabu hiyo Sharik Choughule, Secretary Lion Babul na Rais wao Dk. Hussein Hassan, wengine ni wajumbe wa klabu hiyo wakimkabidhi chakula mgonjwa hospitalini hapo. |
Zoezi la ugawaji likiendelea hospitalini ili kuhahikisha wagonjwa wanapata chakula hicho. |
Mungu awape nafuu Wagonjwa wote waliolazwa Hospitalini hapo, Blog hii inatoa pole kwa Wagonjwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni