Jumamosi, 26 Julai 2014

WANANCHI, DAR ES SALAAM, WAANDAMANA KUUNGANA WENGINE DUNIANI KUPINGA MAUAJI YA YANAYOFANYWA NA ISLAEL, HUKO PALESTINA.


Ni kwa muda gani ulimwengu utaziba masikio yake ili usisikilize umwagaji damu wa Wapelestina mikononi mwa wavamizi?
Je! Wapelestina hawapaswi kufurahia haki yao ya kuishi kwa uhuru katika ardhi yao kama watu wengine?
Uhalisi wa Kimataifa ambao kwa ulilinganiwa na ulimwengu kuutambua na kushikana nao unakanyagwa kila siku katika Palestina na jeshi la wavamizi na ongezeko lake la kijeshi na mazingira yanayowekwa katika miji yao, vijiji, kambi na kusababisha umwagaji damu wa Wapelestina kwa mashine pofu za kijeshi zilizokusudiwa kwa ajili ya kuwaangamiza waislamu na Masjid Al Aqsa.

Wandamanaji wakipinga vitendo vya mauji yanayotokea nchini Palestina pamoja na kukumbuka siku ya Qudus.



Maandamano hayo yalianzia eneo la Boma, Barabara ya Kawawa, Dar es Salaam, kuelekea maeneo ya Kigogo katika msikti wa Masjid Ghadir.


Maandamano hayo pia ni sehemu kumbukumbu ya siku ya Qudus, siku ambayo hukumbukwa kila  mwezi 27, ya mwezi mtukufu wa Ramadhan, kutokana na kuvamiwa kwa msikiti wa Al Aqa ulioko Plaestina ambao umekaliwa na watu wasio waislamu.



Baadhi ya wandamanaji wakiwa katika maandamano ya amani kupinga vitendo vinavyofanywa taifa Islael kkufanya mauaji wa Palestina.



Hakuna maoni: