Jumapili, 27 Julai 2014

AMANI LIONS CLUB, DAR ES SALAAM, IMESAIDIA WATOTO YATIMA NA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.

Amani Lions Klabu ya Dar es Salaam, imetoa msaada wa chakula na mahitaji muhimu kwa Kituo Hisani cha kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.
Msaada huo wenye thamani ya sh. milioni 1.4, ulitolewa, jana, Dar es Salaam, kwa kituo hicho kilichoko Mbagala, Majimatitu ambacho kina watoto 40.
Msaada wa Vyakula uliotolewa ni pamoja na Unga wa Sembe, Maharage, Njugu Mawe, Sukari, Mafuta ya Kula, Biskuti ambapo mahitaji mengine ni Viatu, Nguo, Khanga na Sabuni za Kufuria.
Rais wa Klabu hiyo, Dk. Hasan Hussein akikabidhi msaada huo alisema wameona kuwasaidia watoto hao kutokana kuguswa na maisha wanayoishi na wanahitaji kusaidiwa.
Alisema msaada huo ni sehemu mojawapo ya shughuli za klabu hiyo kusaidia jamii ya watanzania hususan wenye matatizo au kutoa msaada kwa ajili ya maendeleo.
Dk. Hussein alisema jamii inapaswa kusaidiwa ndio maana wao wamekuwa mstari wa mbele katika kusaidia kwa michango itolewayo na viongozi na wanachama wa klabu yao.
Naye Mlezi wa Kituo hicho cha Hisani, Hidaya Shukran alisema msaada huo umekuja wakati muafaka kuokana na mahitaji ya kituo hicho.
Alisema klabu hiyo imekuwa ikishirikiana nayo katika kusaidia mambo mbalimbali katika kituo hicho hivyo waendelee kuwasaidia watoto hao, ili baadae nao waje kuwa na maisha mazuri.


Rais wa Amani Lions Klabu ya Dar es Salaam, Dk. Hasan Husein akizungumza na watoto wa Kituo hicho baada ya kukabidhi msaada wa vyakula na mahitaji mengine yenye thamani sh. milioni 1.4.
Mmoja wa Viongozi wa Amani Lions Klabu ya Dar es Salaam, Sharik Choughle akisalimiana na mlezi wa kituo hicho Bi. Hidaya Shukrani.


Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Hisani cha kulea watoto yatima na wanaishi katika mazingira magumu, kilichopo Mbagala, Majimatitu, Dar es Salaam.

Viongozi wa Amani Lions Klabu ya Dar es Salaam na watoto wa yatima na wanaishi katika mazingira magumu wa kituo cha Hisani wakiomba dua baada kutembelea na kutoa msaada.

Mlezi wa Kituo cha Hisani Orphans Centre Trust, Hidaya Shukrani akishukuru baada ya kupokea msaada wa vyakula kutoka Amani Lions Klabu ya Dar es Salaam.

Jumamosi, 26 Julai 2014

WANANCHI, DAR ES SALAAM, WAANDAMANA KUUNGANA WENGINE DUNIANI KUPINGA MAUAJI YA YANAYOFANYWA NA ISLAEL, HUKO PALESTINA.


Ni kwa muda gani ulimwengu utaziba masikio yake ili usisikilize umwagaji damu wa Wapelestina mikononi mwa wavamizi?
Je! Wapelestina hawapaswi kufurahia haki yao ya kuishi kwa uhuru katika ardhi yao kama watu wengine?
Uhalisi wa Kimataifa ambao kwa ulilinganiwa na ulimwengu kuutambua na kushikana nao unakanyagwa kila siku katika Palestina na jeshi la wavamizi na ongezeko lake la kijeshi na mazingira yanayowekwa katika miji yao, vijiji, kambi na kusababisha umwagaji damu wa Wapelestina kwa mashine pofu za kijeshi zilizokusudiwa kwa ajili ya kuwaangamiza waislamu na Masjid Al Aqsa.

Wandamanaji wakipinga vitendo vya mauji yanayotokea nchini Palestina pamoja na kukumbuka siku ya Qudus.



Maandamano hayo yalianzia eneo la Boma, Barabara ya Kawawa, Dar es Salaam, kuelekea maeneo ya Kigogo katika msikti wa Masjid Ghadir.


Maandamano hayo pia ni sehemu kumbukumbu ya siku ya Qudus, siku ambayo hukumbukwa kila  mwezi 27, ya mwezi mtukufu wa Ramadhan, kutokana na kuvamiwa kwa msikiti wa Al Aqa ulioko Plaestina ambao umekaliwa na watu wasio waislamu.



Baadhi ya wandamanaji wakiwa katika maandamano ya amani kupinga vitendo vinavyofanywa taifa Islael kkufanya mauaji wa Palestina.



Ijumaa, 25 Julai 2014

MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM, ATEMBELEA SHINA LA CCM, LA PAMBA ROAD, DAR ES SALAAM.


Meya Masabuli amehaidi kutoa sh. milioni 5. kuchangia SACCOS ya Shina la Pamba road, ambapo amewashauri waanzishe VICOBA, ili kuweza kujileta maendeleo.
Pia, ameadi kuwa kuwachukulia hatua ba kisheria kwa wae aliojenga na kuziba maitaro hali inayopelekea ksababisha uchafu katikati ya jiji hilo.




Katibu wa Shina hilo akimtambulisha Meya huyo kwa wanachama waliofika kumsikiliza wakati alipotembelea katika shina hilo.


Wanachama wa shina hilo la Pamba road, wakimsikiliza kwa makini Meya, Masabuli wakati akitoa neno kwa wanachama hao.

Masabuli akipokea risala iliyosomwa na Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Kivukoni, Abdallah Isere (Sosi Malema). Kushoto ni Mwenyekiti wa Shina hilo Sharik.

Sosi Malema akisoma Risala kwa mgeni rasmi na kueleza changamoto zao zinazowakabili vijana katika eneo hilo.


Masabuli akikabidhiwa maua na Mwenyekiti huyo.



Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Masabuli akikaribishwa na Mwenyekiti wa Shina la CCM, Pamba road, Dar es Salaam, Sharik Choughule baada ya kutembela katika shina hilo.

Jumanne, 22 Julai 2014

BENKI YA WATU WA ZANZIBAR (PBZ), IMEFUTURISHA WAFANYAKAZI NA WATEJA WAKE, DAR ES SALAAM.

Gavana wa BoT, Juma Reli aipongeza Benki ya Watu wa Zanzibar kwa kutoa huduma bora kwa wateja kwa haraka na ufanisi pamoja kutoa huduma zinazolingana na hali halisi ya wateja wao.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki hiyo, Said Said, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ, wakati wa hafla hiyo futari alisema amana ya benki hiyo imekuwa ikiongezeka kutoka asilimia 30 hadi 40, ambayo ni kubwa ukilinganisha na soko la mabenki.
 Said alisema PBZ, iko katika hatua za mwisho kufungua matawi mengine manne, yatakayoendeshwa kwa mfumo huo, pamoja kuborsha huduma kwa wateja wao.
Aidha, Said alisema benki hiyo imerahisisha huduma kwa wateja kwani wanaweza kutumia mtandao wa intanet na simu ya mkononi pamoja na kusafirisha fedha kutoka nje ya nchi kwa wateja wanaoishi nje ya nchi.


Wafanyakazi na wateja wa benki hiyo wakiwa katika hafla hiyo.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Juma Reli akiwaongoza wafanyakazi na wateja wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), katika futari iliyoandaliwa na Benki PBZ. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya PBZ, Abdulrahaman Mwinyi Jumbe na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Benki hiyO Said Said.



Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymound Mushi akiwa katika futari uliyoandaliwa na PBZ.


WATU WANANE WANASHIKILIWA KUTOKANA NA TUKIO LA KUKUTWA KWA VIUNGO VYA BINADAMU, ENEO LA BUNJU, DAR ES SALAAM.

KAMISHNA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akielezea kuhusu tukio la kutupwa viungo vya binadam katika bonde la Mbweni Mpiji, eneo la Bunju, Dar es Salaam. 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dara es Salaam, limebaini kuwa viungo vya binadamu vilivyokutwa eneo la bonde la Mbweni Mpiji, kata ya Bunju, Dar es Salaam, kwa mara ya mwisho vilikuwa katika maabara ya Chuo Kikuu cha Madaktari (IMTU).
Polisi linawashikilia watu wanane wakiwemo madaktari wa IMTU kwa ajili mahojiano kwani inasadikiwa kuhusika na kuweko kwa viuongo hivyo.
 Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar e Salaam, Suleiman Kova alisema chuo hicho hufanya mafunzo ya udaktari kwa vitendo.
Alisema Jeshi hilo limeunda jopo maalumu la wapelelezi kwa ajili ya kuchunguza tukio la kuweko kwa vifaa hivyo ambapo limewashikilisha Mkuu wa Upelelezi wa Kanda hiyo ACP, Japhari Mohamed kwa kusaidiana na Daktari wa Jeshi la Polisi anayehusika na masuala ya uchunguzi wa miili ya binadamu na madaktari wengine kutoka katika Hoaspitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Tukio hilo lilitokea juzi katika eneo la Bunju, ambapo viungo vya binadamu vilikutwa katika mifuko ya plastic 85, ambapo ndani yake kulikuwa na Vichwa, Miguu, Mikono, moyo mapafu, vifua na mifupa mbalimbali ikiwa vimekaushwa na havikuwa na uvundo.
Pia, katika eneo hilo kulikutwa vifaa vya kufanyia operesheni ikiwemo nguo malum (Apron) 20, mipira ya kuva mikononi pamoja na karatasi ya maswali na majibu.

Jumapili, 20 Julai 2014

LIONS CLUB OF AMAN YATOA MSADA WA CHAKULA, KWA WAGONJWA 300, KATIKA TAASIS YA OCEAN ROAD, DAR ES SALAAM.

KLABU ya Amani Lions, imetoa msaada wa chakula kwa wagonjwa zaidi ya 300, katika Hospitali ya Saratani ya Ocean road, jijini, Dar es Salaam.
Rais Mteule wa Klabu hiyo, Dk. Hussein Hassan, alizema lengo la msaada huo ni kuwajali watu wenye matatizo ili nao wajione sehemu ya jamii.
Alisema msaada huo ni sehemu mojawapo ya shughuli za za klabu hiyo katika kusaidia jamii kwa kuwa saidia miradi mbalimbali ya kijamii.
"Tumekuwa tukisaidia watu wenye ulemavu, watoto wa mitaani, wajane, kugawa miwani kwa wenye matatizo ya macho, kuanzisha miradi ya maendeleo  pamoja kufanya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali", alisema.
  Aidha, alisema klabu hiyo imeambatana na wajumbe wake wakiwemo wawili kutoka nchini marekani ambao wako nchini kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na klabu hiyo.
Pia, Hussan alisema wanatarajia kupokea msaada wa  jozi 400 ya miwani ya macho kutoka kwa wajumbe hao, ambapo msaada huo utatolewa kwa jamii.

Chakula kikipakuliwa kwa ajili kusambaza kwa wagonjwa waliorazwa hospitalini hapo.


Rais wa Lions Club, Dk. Hussein Hassan akiwaongoza wanachama wenzake katika kupakua chakula hicho ambacho kiligawiwa kwa wagonjwa 300.


Mgonjwa akipewa chakula kutoka kwa mwanachama wa klabu ya Lions klabu ya Aman hospitalini hapo.

Kulia ni Director wa Klabu hiyo Sharik Choughule, Secretary Lion Babul na Rais wao Dk. Hussein Hassan, wengine ni wajumbe wa klabu hiyo wakimkabidhi chakula mgonjwa hospitalini hapo.

Zoezi la ugawaji likiendelea hospitalini ili kuhahikisha wagonjwa wanapata chakula hicho.











Mungu awape nafuu Wagonjwa wote waliolazwa Hospitalini hapo, Blog hii inatoa pole kwa Wagonjwa.

Jumanne, 15 Julai 2014

MBRAZIL MWINGINE ATUA YANGA...

Genilson Santana Santos.
Mshambulaji kutoka nchini Brazil ametua katika Mkao Makuu ya klabu hiyo iloko mitaa ya Twiga na Jangwani kwa ajili kujiunga na klabu hiyo ambayo imepanga kuwa ya kimataifa.
 Santos, alitua katika ardhi ya Tanzania akitokea kwao saa 8.15, mchana ambapo alipokewa na viongozi mbalimbali wa klabu hiyo huku akilakiwa na wanachama wa yanga, ambapo alipelekwa moja kwa moja hadi klabuni hapo.
 Huyo ni mchezaji wa pili kutia katika klabu hiyo ambapo wakwanza Kiungo mshambuliaji,  Marcel Ferreira Coutinho.


Genilson Santana Santos, akiwasili katika Makao Mkauu ya Klabu ya Yanga kwa ajili ya kuingia kandarasi ya kuitumikia klabu hiyo.

Nimekuja kuwashika

Genilson Santana Santos.

Akisaini kitabu cha wageni klabuni hapo.

Afisa Habari wa Klabu ya Yanga baraka Kizuguto, akimkaribisha Santos, klabuni hapo.


Akiwasalimia baadhi ya wanachama na mashabiki wa Yanga.


Binda akizumtambulisha Santos baada kukanyaga katika klabuni hapo.


Wanachama na Mashabiki wa klabu ya Yanga wakiwa klabuni hapo kumwangalia Santos.


Jumamosi, 12 Julai 2014

SHARI K MWENYEKITI MPYA SHINA LA CCM, PAMBA ROAD, DAR ES SALAAM.

Mwenyeki wa mpya wa shina la  Wakeleketwa CCM, Pamba road, Sharik Choughule amesema atahakikisha chama hicho kinashinda chaguzi za serikali za mtaa na uchaguzi wa mkuu wa 2015.
Choughule alisema hayo juzi baada ya kuchaguliwa mwenyekiti mpya wa shina hilo katika uchaguzi uliofanyka katika ukumbi wa Karemjee, Dar es Salaam.
 Alisema kazi iliko mbele yake ni kuhakikisha kukiletea chama  maendeleo pamoja kuendeleza umoja uliko ndani ya shina hilo liloko katikati ya jiji la Dar es Salaam, maeneo ya Posta.
"Siwezi kuongea maneno mengi ila vitendo vyangu vitaonekana kwa kuiletea CCM, maendeleo na tawi shina letu, suala la msingi ni kushirikiana na wanachama wenzangu, kwani nina uzowefu wa uongozi kutokana na kuwa Kamanda wa Vijana Kata ya Kivukoni", alisema Choughule.

Sharik akwa na mpinzani wake kabla ya uchaguzi ndani ya ukumbi wa Karemjee, Dar es Salaam.


Wagombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Shina la CCM, Pamba road wakiwa mbele ya wapiga kura kabla ya kila mmoja kuomba kura.

Mwenyekiti  mpya wa Shina la Pamba Road Sharik Choughule akiwa mwenye furaha baada ya kumalizika kwa kuhesabiwa kura.

Wanachama wakipiga kura katika uchaguzi huo.
Akitangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa tawi hilo.

Akipongezwa na mpinzani wake aliyechuana naye katika uchaguzi uliomuweka madarakani Shariki, ambaye pia ni Kamanda wa Vijana, CCM, Kata ya Kivukoni.

Akikabidhiwa kiti rasmi na mwenyekiti wa uchaguzi, kulia ni Katibu wa shina.

Mwenyekiti mpya akinyanyuliwa juu juu 





Akisalimia wanachama akiwa makao Makuu ya Shina hilo la Pamba road, maeneo ya Posta, Dar es Salaam.

Mgombea aliyejitoa katika hatua za mwisho akipiga kura yake.