Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha CETRADIN Saum Rashid kulia akizungumzia kuhusu Amani |
KITUO cha Mafunzo na Maendeleo (CETRADIN) kimewataka
vijana wasikubali kutumiwa na wanasiasa kuwa mtaji wa
kuvuruga amani katika kipindi hichi cha kupata katiba mpya.
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Saum Rashid alisema
vitendo vyote vinavyoashiria uvunjifu wa amani katika kupata
katiba mpya.
Alisema amani inapovunjika katika nchi yeyote wanaoathirika
zaidi ni wanawake, watoto wazee na walemavu, hivyo basi
amewataka vijana kuweka utaifa mbele ili kuindeleza amani
iliyodumu kwa miaka mingi.
"Katiba ya kweli na yenye maslai kwa watanzania haiwezi
kupatikana kwa maandamano wala kupambana na vyombo vya
usalama, ila katiba mpya itapatikana endapo kutakuwa na
maridhiano na kuweka utaifa mbele." alisema.
Mkurugenzi huyo alisema wanaimani Rais Jakaya Kikwete
ataufikisha mwisho mchakato wa kupata katiba mpya kwa
wakati kwakua ni msikivu na mwadirifu hivyo basi watanzania
wampe nafasi.
Aidha, CETRADIN imemuomba Rais Kikwete watakapokutana
na vyama vya siasa wamalize kasoro zilizokuwepo katika
mchakato huo wa katiba mpya ili kudumisha amani iliopo kwa
watanzania na kuendelea kuwa mfano bora katika Afrika.
Hata hivyo, wamemuomba Rais amani na mafanikio ya katiba
ijayo kuwe na ushiriki sawa kati ya wanawake na wanaume
katika bunge maalum lakatiba, kwani wanaamini suala hilo liko
ndani ya uwezo wake.
Maoni 1 :
Nimeona mtaalam.
Chapisha Maoni