Jumatatu, 14 Oktoba 2013

CENTRE FOR TRADING & DEVELOPMENT INITIATIVE (CETRADIN)

CETRADIN: VIJANA WASIKUBALI KURUBUNIWA NA WANASIASA KUVURUGA AMANI YA NCHI KATIKA KIPINDI HICHI CHA MCHAKATO WA KATIBA...



Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha CETRADIN Saum Rashid kulia akizungumzia kuhusu Amani
 
KITUO cha Mafunzo na Maendeleo (CETRADIN) kimewataka

vijana wasikubali kutumiwa na wanasiasa kuwa mtaji wa

kuvuruga amani katika kipindi hichi cha kupata katiba mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Saum Rashid alisema

wameamua kuungana na wanawake wote nchini kulaani

vitendo vyote vinavyoashiria uvunjifu wa amani katika kupata


katiba mpya.


Alisema amani inapovunjika katika nchi yeyote wanaoathirika

zaidi ni wanawake, watoto wazee na walemavu, hivyo basi

amewataka vijana kuweka utaifa mbele ili kuindeleza amani

iliyodumu kwa miaka mingi.


"Katiba ya kweli na yenye maslai kwa watanzania haiwezi


kupatikana kwa maandamano wala kupambana na vyombo vya


usalama, ila katiba mpya itapatikana endapo kutakuwa na

maridhiano na kuweka utaifa mbele." alisema.

Mkurugenzi huyo alisema wanaimani Rais Jakaya Kikwete

ataufikisha mwisho mchakato wa kupata katiba mpya kwa

wakati kwakua ni msikivu na mwadirifu hivyo basi watanzania

wampe nafasi.

Aidha, CETRADIN imemuomba Rais Kikwete watakapokutana

na vyama vya siasa wamalize kasoro zilizokuwepo katika

mchakato huo wa katiba mpya ili kudumisha amani iliopo kwa

watanzania na kuendelea kuwa mfano bora katika Afrika.

Hata hivyo, wamemuomba Rais amani na mafanikio ya katiba

ijayo kuwe na ushiriki sawa kati ya wanawake na wanaume

katika bunge maalum lakatiba, kwani wanaamini suala hilo liko

ndani ya uwezo wake.

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

Nimeona mtaalam.