Ijumaa, 25 Oktoba 2013

WANNE WAJIUNGA NA NCCR -MAGEUZI

CHAMA cha NCR-Mageuzi leo kimeongeza wanachama wapya wanne baadhi yao ni viongozi wa vyama mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari, makao makuu chama hicho, yako Illa mtaa wa Arusha jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu Mosena Nyambabe alisema wanachama leo tunawapa kadi rasmi na kijiunga na NCCR Mageuzi.

Aidha, Nyambabe aliwatambulisha wanachama hao wapya ni Ramadhani Manyeko, kutoka chama cha APPT-Maendeleo, ambaye alikuwa katibu wa Mkoa wa Tanga, Mchata Erick Mchata kutoka chama cha Saut ya Umma (SAU), ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Florence Abdallah Twalipo, kutoka CCM na Lilian Kifunga kutoka CHADEMA.

Katika hatua nyingine katibu huyo amewakumbusha baadhi ya viongozi wa majimbo ambayo hawajafanya uchaguzi, wafanye uchaguzi wao, kwani wako katika hatua za mwisho kuandaa uchaguzi mkuu.

Hata hivyo aliwapongeza majimbo ambayo yameshakamilisha zoezi la uchaguzi kwani majimbo 206 teyari yameshafanya uchaguzi kati ya 239 ya Tanzania Bara na Zanzibar, hivyo basi majimbo ambayo bado yafanye chaguzi kabla ya Novemba 10, 2013.

Pia, Nyambabe alitoa pole kwa wanahabari kwa kufiwa na mwanahabari mkongwe nchini Julius Nyaisanga, Maarufu Uncle J, ambaye alifariki 20, mwezi huu, Mkoani Morogoro.

Alisema NCCR mageuzi watamkumbuka kutokana na utendaji wake wa kazi na uadirifu wake...,pia alitoa pole kwa na kumtakia afya njema mwandishi wa habari wa kituo cha ITV Ufoo Saro.

Hakuna maoni: