Ijumaa, 25 Oktoba 2013

MOTO ULIVYOTEKETEZA GHALA LA KUHIFADHIA MIPRA YA KUTENGENEZEA VIATU KATIKA KIWANDA CHA OK PLASTIC


MKAZI wa Vingunguti, Dar es Salaam, hakufahamika jina lake amesababisha kuchoma moto mabaki ya kutengenezea viatu ya kiwanda cha Ok Plastic kilichoko Vingunguti.

Mtu huyo ambaye hakufahamika jina lake inasadikiwa alikuwa analina asali katika eneo la kuhifadhia mabaki hayo, ambapo aliwaona nyuki wakizagaa katika eneo hilo.

Kaimu Kamanda wa Temeke Kikosi cha Zimamoto Hamisi Rutengo alisema moto ulianza saa 4.15 asubuhi, ambapo ulisababishwa na kijana huyo aliyekuwa akitaka kulina asali baada ya kuona nyuki katika eneo hilo.

Rutengo alisema mtu huyo aliwasha moto, hata hivyo alishindwa kuudhibiti na kuenea sehemu mbalimbali na kuanza kuteketeza mabaki ya mapira ambayo yalikuwa yamehifadhiwa kwa lengo la kutengenezwa tena.

Kwa mujibu wa Kamanda alisema mtu huyo anashikiriwa katika kituo cha polisi Buguruni kwa ajili uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto.

Kwa upande wa Afisa Utawala wa kiwanda cha Ok Plastic Martine Msamba alisema mlinzi wao alimuona mtu akizagaa katika eneo huku akiwa amewasha moto.


Alisema mlinzi alienda kumuamuru auzime moto na aondoke katika eneo hilo laikini mtu huyo alikataa ndipo mlinzi alienda kuomba msaada kwa walinzi wenzake ili wamtoe kijana huyo.

Msamba alisema baada ya kurudi katika eneo hilo walikuta moto umeshaenea sehemu kubwa, walimkamata kijana huyo na kumkabidhi kwa vyombo vya usalama waliokuwa wanafanya doria katika eneo hilo.

Hata hivyo Afisa huyo alisema eneo hilo lilikuwa mali yao lakini kwa sasa si mali kiwanda, hivyo wamekuwa wakiyaondoa mabaki hayo kidogokidogo katika eneo hilo.

Hakuna maoni: