Jumatatu, 21 Oktoba 2013

SHULE YA MSERU imeipongeza serikali kwakuweka alama mpya usahihishaji wa mitihani ya kidato cha nne ,mwaka huu mitihani itaanza mwezi ujao.

Wanafunzi wa Mseru Sekondali wakiwa katika mafali.

MKUU wa shule ya Sekondali Mseru, Fabianus Kapinga amesema alama mpya zitakazotumika katika kusahihisha wa mitihani ya kidato cha nne mwaka huu itasaidia kuinua kiwango cha elimu nchini.

Kapinga alisema hayo, Kongowe, wilayani Mkuranga, mwishoni mwa wiki wakati wa mahafali ya shule hiyo ambapo alisema alama F, itaanzia 0 hadi 34, waka
ti awali ilikuwa alama F inaanzia 0 hadi 20.

"Waziri wa elimu Dk. Shukuru Kawambwa katika hotuba yake kwa wakaguzi wa shule alisema anataka kuona mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) unafanikiwa katika kuinua kiwango cha elimu." alisema.

Aidha, Kapinga alisema kwa upande wa shule ya mseru imeweka mikakati ya kuinua ufaulu kwa wanafunzi ambapo wanafunzi waliofeli mitihani ya kidato cha kwanza mwaka huu watarudia tena kidato cha kwanza mwakani.

Alisema mikakati mingine ni kuhakikisha kwamba kila mwanafunzi anakuwa jarada la kutunzia taarifa za mitihani yake ili awe na kumbukumbu ya maswali.

Alisema mwanafunzi atapewa maswali ya kufanya wakati wa likizo ambapo msimamizi atakuwa mzazi wake na atakaporudi shuleni jarada hilo litakaguliwa na endapo itabainika hajafanya maswali aliyopewa atarudishwa nyumbani.

Hata hivyo amewataka wazazi kuhakikisha wanawalipia watoto wao ada kwa wakati ili kukabiliana na changamoto zilipo katika shule hiyo.

Kapinga alisema wazazi tunawadai sh. milioni 11.6 kwani shule ina wanafunzi 217, kati ya hao 31, ndio wanaolipa ada kamili, wanafunzi 57, wanalipa nusu ada na 129 wanafadhiliwa na shule hiyo.
Wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Mseru sekondali wakiimba katika mafali yaliofanyika katika shule hiyo ilioko Kongowe, Mkuranga Mkoani Pwani. 

Hakuna maoni: