Karibu katika ulimwengu wa habari.Hapa utapata habari mbalimbali kukuelimisha, burudisha na kuwa wa kwanza kabisa kujua mambo mbalimbali.
Jumamosi, 19 Oktoba 2013
KANISA LA CHRIST EMBASSY KUTOKA NIGERIA LAKARABATI KITUO CHA POLISI CHA OYSTERBAY
KANISA la Christ Embassy limewataka wananchi kutii sheria za nchi na kuachana kufanya vitendo vya uharifu katika jamii.
Mchungaji wa kanisa hilo Ken Igini alitoa wito huo wakati wa sherehe za ufunguzi jengo la kituo cha polisi cha Oysterbay lililofanyiwa ukarabati wa kupakwa rangi na kanisa hilo.
Alisema utawala bora katika nchi ni pamoja kulinda usalama wa watu, ambapo jeshi la polisi limekuwa likitekeleza majukumu yake ipasavyo ndio maana kanisa hilo limekuwa likifundisha upendo na amani kwa watu wote.
Aidha, Mchungaji huyo alisema mradi huo wa kukarabati kituo hicho ni mojawapo ya sera za kanisa hilo kutambua na kuheshimu umuhimu wa huduma zitolewazo na jeshi la polisi kwa kuliinda jamii na mali zako.
Pia, alisema kanisa hilo linauunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha jeshi la polisi linafanya kazi katika mazingira mazuri ndio maana na wao wameweza kulikabarati jengo hilo.
Mchungaji Igini alisema kanisa hilo lina matawi duniani kote ikiwemo Tanzania ambapo kuna matawi 14, ambapo wamekuwa wakijihusisha kufundisha upendo na amani kwa watu wote.
Naye Mkuu wa Polisi Wilayani Kinondoni Wibrod Mutafungwa alisema kanisa hilo limeonyesha mapenzi kwa kituo hicho cha Oysterbay hivyo wameshukuru kwa ukarabati huo.
Mutafungwa aliziomba taasisi nyingine kujitolea katika kulisaidia jeshi la polisi nchini kutokana na kazi kubwa wanayoifanya ya kulinda watu na mali zao
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni