Ijumaa, 25 Oktoba 2013

CHUO CHA SERIKALI ZA MITAA, DODOMA CHAONGEZA UDAHILI KWA WANAFUNZI

AFISA Uhusiano wa Chuo cha Serikali za Mitaa Sebera Furgece akizungumza na waandishi wa habari kuhusu chuo hicho kuongeza udahili kwa wanafunzi kwa mwaka 2013/2013.


CHUO cha Serikali za Mitaa kilichopo Hombolo Mkoani Dodoma kimeongeza udahili kwa wanafunzi na kufikia 2,491, ikiwa ni pamoja wale wanaoendelea na masomo kwa mwaka 2013/2014.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), jijini Dar es Salaam, Afisa Uhusiano wa chuo hicho Sebera Furgece alisema idadi hiyo inajumuisha wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na cha sita, ambao wanaojiunga na Stashahada na Astashada katika fani mbali mbali.

Alisema idadi hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia 96.5...aidha chuo hicho kimeanza ujenzi wa kituo cha Afya kitakachogharimu sh. bilioni 7.6, ambapo lengo la kuanzisha kituo hicho ni kuboresha utoaji huduma za Afya kwa wagonjwa wapatao 3000.

Madhumuni ya chuo hicho ni kuchangia uwezeshaji wa mchakato wa kupeleka madaraka kwa wananchi, kujenga na kukuza utawala bora, kukuza uchumi na kuondoa umaskini katika ngazi mbalimbali za serikali za mitaa hapa nchini.

Hakuna maoni: