Jumamosi, 12 Oktoba 2013


ICC: SENUSSI AFUNGULIWE MASHTAKA LIBYA.

Gaddafi enzi za uhai wake
Mahakama ya kimataifa ya jinai, ICC, imeamua aliyekuwa Mkuu wa Ujasusi enzi ya utawala wa marehemu Muamar Gadaffi, Abdullah al-Senussi, mashtaka yake yafunguliwe nchini Libya.

ICC haitaendelea kumtaka Bwana Senussi kwenda The Hague kwa ajili tuhuma zinazomkabili dhidi yake.

Senussi aliyekuwa mkuu wa ujasusi alitakikana na mahakama ya ICC kwa uhalifu dhidi ya binadamu , makosa aliyoyafanya wakati wa mapinduzi ya kiraia dhidi ya Gaddafi.

Mkuu huyo alikabidhiwa na Mauritania kwa Libya baada ya kukamatwa nchini humo mwaka jana.

ICC kwa kawaida haiendeshi kesi dhidi ya mshukiwa ikiwa kuna dalili kwamba watatendewa haki nchini mwao.

Aidha, taarifa ya mahakama hiyo imesema kuwa uamuzi huo hauna uhusiano wowote na kesi dhidi ya mwanawe marehemu Gaddafi,Saif al-Islam Gaddafi anayetakiwa na mahakama hiyo.

Islam pia alishtakiwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita na alishitakiwa pamoja na watu wengine 36.

Saif Gaddafi anazuiliwa na kundi la wapiganaji wa kiisilamu mjini Zintan. Mwezi jana wapiganaji hao, walikataa kumkabidhi Seif kwa serikali kufikishwa mahakamani na Senussi .

Hakuna maoni: