Karibu katika ulimwengu wa habari.Hapa utapata habari mbalimbali kukuelimisha, burudisha na kuwa wa kwanza kabisa kujua mambo mbalimbali.
Jumatatu, 5 Mei 2014
AWAMU YA KWANZA WA MRADI WA MABASI YAENDAYO HARAKA, JIJINI DAR ER SALAAM, KUKAMILIKA MWAKA HUU.
Akizungumza, jijini Dar es Salaam, Meneja uendeshaji wa DART, Peter Munuo aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maendeleo mradi huo.
Munuo alisema wanatarajia kuanza kutoa huduma ya mpito Desemba mwaka huu ambapo mwakani huduma kamuli itaanza rasmi.
Alisema kwa kipindi hiki cha huduma mpito mabasi ya Meneja huyo alisema hayo mabasi ya majaribio yana uwezo wa kubeba abiria ya 140 hadi 160 hadi watakapoanza kutoa huduma kamili ifikapo mwaka 2015, hivyo yatasaidia kupunguza msongamano wa watu unaosababishwa na shida ya usafiri.
Alisema kwa mujibu wa tafiti ambazo wamezifanya ndani na nje ya nchi, imebainika kuwa mfumo wa mabasi yaendayo kasi ndiyo unaoweza kupunguza msongamano wa watu na tatizo la usafiri.
Jumapili, 4 Mei 2014
SERIKALI IMEOMBWA KUONGOZA ULINZI KWA WATU WENYE UALBINO KATIKA MIKOA YA KANDA YA ZIWA.
Pia, imetakiwa kutenga bajeti maalum kwa ajili ya kupambana na saratani ya ngozi kwa watu wenye ualbino kwa kutoa kinga, tiba na mafunzo.
Hayo yalisemwa na Mjumbe wa Chama cha Albino Tanzania Husein Kibindu wakati akisoma risala Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Seif Rashid, kwenye maadhimisho ya siku ya Ualbino, katika viwanja vya Mnazimoja, Dar es Salaam, jana.
Kibindu alisema kuanzia mwaka huu kumekuwa na taarifa za matishio kwa akina mama na watoto wenye ualbino katika mikoa ya kanda ya ziwa, ambapo sababu kubwa ikielezwa kuwa ni imani potofu za kishrikina.
Alisema imani potofu kwa upande wa mikoa hiyo imekuwa iko juu, ambapo kuna mikasa ya mauaji ya watu wenye ualbina na wasiokuwa ualbino, wakiwemo wanawake na watoto.
Aidha, Kibindu alisema vitendo vya mauaji na uakataji wa viungo kwa watu wenye ualbino unapelekea watu na familia zao kupata madhara ya kisaikolojia na kwasababishia umaskini kutokana na kupoteza viungo vya miili yao.
| WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Jeshi la Wokovu Kurasini jijini, Dar es Salaam, wakiwa katika viwanja vya Mnazimoja, wakati wa maadhimisho hayo, ambayo kitaifa yalifanyika jijini Dar es Salaam. |
| KIKUNDI cha sanaa cha Ualbino wakitoa burudani mbele ya wananchi waliofika katika siku hiyo ya maadhimisho. |
2000, WASADIKIWA KUFA HUKO KASKAZINI, KASKAZINI MASHARIKI, NCHINI AFGHANISTAN.
![]() |
| Baadhi walipanda kwenye paa kusubiri msaada wa uokoaji |
Vijiji hivyo vimefunikwa na udongo wenye ukubwa wa karibu mita 10, kwenda juu baada ya eneo la mlima mmoja kuporomoka kutokana na mvua kubwa zinazonyesha.
Miili ya watu wapatao 350 imepatikana katika maporomoko ya ardhi kaskazini mashariki mwa taifa hilo na hakuna mtu yoyote aliyepatikana akiwa hai.
Aidha, taarifa kutoka Umoja wa Mataifa (UN) zinasema karibu watu 4000 hawana makazi, ambapo juhudi za uokoji zinaendelea siku ya pili.
![]() |
| Mvua zilizonyesha na kusababisha mafuriko na kuleta madhara kwa wananchi wa Afghanstan |
Ijumaa, 2 Mei 2014
WATU 19, WAMEUWA BAADA YA KUTOKEA MLIPUKO KATIKA MJI KUU WA NIGERIA, ABUJA.
![]() |
| Baadhi ya watu waliojeruhiwa katika mlipuko huo. |
Mlipuko huo ulitokea katika eneo la Nyanya, karibu na kituo cha basi ambako zaidi ya watu 70 waliuwawa katika shambulizi la tarehe14 mwezi Aprili.
Waandishi wanasema kuwa mlipuko huo umesababishwa na bomu lililotegwa ndani ya gari. Mmoja wa walioshuhudia kisa hicho amesema aliona miili 20 ya watu waliouwawa.
Hakuna kundi lililodai kuhusika katika shambulizi hilo lakini kundi la wanamgambo wa kiislamu la Boko Haram limewahi kutekeleza mashambulizi kama hayo mjini Abuja
Mengi ya mashambulizi ya Boko Haram yamekuwa yakitokea katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria, lakini shambulizi la bomu la Aprili 14, lilizua hofu kwamba huenda wanamgambo hao wameanza kupanua maeneo wanayoendeleza harakati zao.
Alhamisi, 1 Mei 2014
WASICHANA 6000, MTWARA KUNUFAIKA NA MRADI WA HAKUNA WASICHOWEZA BAADA YA KUPATA ELIMU NA MISAADA YA VIFAA VYA KUJISITIRI WAKATI WA HEDHI.

Wasichana mkoani Mtwara wamenufaika na elimu ya afya pamoja na vifaa vitakavyowasaidia kujisitiri wakati wa hedhi.
Elimu hiyo na msaada vimetolewa kupitia mradi wa ujulikanao Hakuna Wasichoweza unaotekelezwa na
asasi ya T-MARC Tanzania kwa ufadhili wa watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la Kimarekani
USAID kwa ushirikiano na Vodacom Foundation.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo kwa wasichana walengwa wa mradi, Meneja wa Mradi wa huo, Doris Chalambo alisisitiza umuhimu wa kuwawezesha wasichana kama njia ya
uhakika ya kufanikisha maendeleo ya jamii na Taifa.
‘’Awamu ya kwanza ya mradi huu imewafikiwa jumla ya wasichana 5000 katika shule za msingi za Mtwara na jumla ya wasichana 1000 walioko nje ya shule katika kata 17", alisema Doris.
Walengwa wa mradi huu ni wasichana wenye umri wa miaka 9 – 15. Jumla ya shule 24 zimefikiwa na mradi huu ambao pia umetoa mafunzo kwa walimu 40 wa shule na Wakunga wa jadi, makungwi/Nyakanga 34 wanaotoa elimu kwa wasichana wanaobalehe.
Pia alisisitiza kwamba elimu hii juu ya masuala ya hedhi itawezesha kuongeza uelewa wa jamii kwa ujumla juu ya umuhimu wa kuwasaidia wasichana ili waweze kuhudhuria masomo yao kwa ufanisi zaidi na kufikia malengo yao kimaisha.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule alisema kuwa
elimu inayotolewa na mradi na mradi huo utaliwezesha Taifa kupunguza kasi ya maambukizi ya
mgonjwa ya kujamiiana ikiwemo maambukizi ya Virusi vya vinavyosababisha Ukimwi (VVU),
miongoni mwa vijana.
Mwakifulefule alisema kila msichana atakuwa akipatiwa pakiti mbili za vifaa hivyo kwa mwezi na zoezi hili litafanyika kwa muda wa miezi mitano mfululizo.
“Tunajivunia kuwa sehemu ya chachu ya maendeleo katika sekta ya elimu hususani mradi huu wa
Hakuna Wasichoweza ambao umelenga kunufaisha jumla ya wasichana 6000 waliopo na wasiopo
shuleni”, alisema Mwakifulefule.
Naye Mtaalamu wa Masuala ya Misaada kwa jamii kutoka Vodafone, Laura Turkington alisema mradi
unakuza ushiriki wa wadau mbali mbali katika kukuza viwango vya elimu pamoja na kutoa taarifa
sahihi kwa jamii kuhusu changamoto zinazowakabili wasichana katika kipindi cha balehe.
Aidha, T-MARC imetoatoa shukurani kwa Shirika la USAID ambalo limetoa msaada wa dola za
Kimarekani laki mbili (200,000) kufadhili uanzishwaji wa mradi huu pamoja na Vodacom
Foundation ambayo imechangia shilingi milioni 160, kufanikisha awamu hii ya kwanza ya mradi.
![]() |
UKAWA WALIVYOWASHA MOTO KISIWANI ZANZIBAR
VIONGOZI Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), jana walifanya mkutano wao wa kwanza katika eneo la Kibanda maiti, mjini Zanzibar.
MWANASIASA MAARUFU WA CHAMA CHA SINN FEIN, GERRY ADAMS, AKAMATWA KASKAZINI IRELAND.
JESHI la Polisi nchini Kazkazini Ireland wamemkamata mwanasiasa mashuhuri wa chama
cha Sinn Fein, Gerry Adams kwa kuhusishwa na mauaji yaliyotokea zaidi ya miaka 40 iliyopita.
Adams anahojiwa kuhusu mauaji ya Jean McConville ambaye alitekwanyara na kundi la waasi
la IRA mnamo mwaka 1972 na kisha akapatikana amepigwa risasi na kuuawa .
Kiongozi huyo amekanusha kuhusika kivyovyote vile akisema kuwa alijipeleka binafsi kuzungumza na
polisi ilikujaribu kusuluhisha madai hayo yaliyomwandama kwa miaka mingi mno .
Adams anakanusha kuhusika kwa vyovyote vile na utekaji nyara wala mauaji yake bi Mc Conville
ambaye alikuwa mama wa watoto 10 .Madai hayo yanafwatia mahojiano mjini Belfast
mwaka wa 2001-2006 baina ya chuo kikuu cha Boston Marekani na wakereketwa wa vita hivyo
vilivyonuiwa kuikomboa Ireland kutoka kwenye minyororo ya ukoloni.
Mahojiano hayo yalifanywa kwa misingi kuwa yangewekwa siri hadi baada ya vifo vya wahusika
wakuu, lakini baada ya kesi za kutaka kutambulika wahusika na wahasiriwa waliotoweka wakati wa
vita hivyochuo hicho kililazimishwa kutoa sehemu ya mahojiano kwa serikali ya Ireland.
Mmoja kati ya watu 16 waliosemekana kutoweka ni Mc Conville, hata hivyo mjane huyo alilaumiwa na
IRA kuwa mpelelezi wa polisi lakini baada ya ufafanuzi wa polisi yapata mwaka wa 1999, ambapo
McConville ilibainika hakuwa.Kundi hilo la IRA lilikiri kutekeleza mauaji yake bi
McConville mwaka wa 1999 lakini mwili wake ulipatikana mwaka wa 2003 ukiwa umetupwa
kwenye ufukwe wa bahari.IRA inashtumiwa kwa kampeini na mauaji
yaliyotikisa Ireland kaskazini kwa takriban miaka 30.
Chanzo: BBC SWAHILI.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)






