Ijumaa, 28 Agosti 2015

Shirika la Afya Dunian (WHO), limetoa msaada wa Dawa za kutakasa mazingira na kutibu maji ili kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu katika mkoa wa Dar es Salaam.

Wakazi wa Dar es Salaam, wametakiwa kuhakikisha wanazingatia kanuni za usafi ili kudhiti kuenea kwa ugonja wa Kipindupindu, ambapo umekuwa ukienea sehemu nyingi jijini humo.

Pia ugonjwa huo umueikumba mkoa wa Pwani ambapo hadi sasa wagonjwa saba wamekuwa wakipatiwa matibabu. Kati ya hao mmoja ameripotiwa kufariki dunia.

Hakuna maoni: