Amani Lions Klabu ya Dar es Salaam, imetoa msaada wa chakula na mahitaji muhimu kwa Kituo Hisani cha kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.
Msaada huo wenye thamani ya sh. milioni 1.4, ulitolewa, jana, Dar es Salaam, kwa kituo hicho kilichoko Mbagala, Majimatitu ambacho kina watoto 40.
Msaada wa Vyakula uliotolewa ni pamoja na Unga wa Sembe, Maharage, Njugu Mawe, Sukari, Mafuta ya Kula, Biskuti ambapo mahitaji mengine ni Viatu, Nguo, Khanga na Sabuni za Kufuria.
Rais wa Klabu hiyo, Dk. Hasan Hussein akikabidhi msaada huo alisema wameona kuwasaidia watoto hao kutokana kuguswa na maisha wanayoishi na wanahitaji kusaidiwa.
Alisema msaada huo ni sehemu mojawapo ya shughuli za klabu hiyo kusaidia jamii ya watanzania hususan wenye matatizo au kutoa msaada kwa ajili ya maendeleo.
Dk. Hussein alisema jamii inapaswa kusaidiwa ndio maana wao wamekuwa mstari wa mbele katika kusaidia kwa michango itolewayo na viongozi na wanachama wa klabu yao.
Naye Mlezi wa Kituo hicho cha Hisani, Hidaya Shukran alisema msaada huo umekuja wakati muafaka kuokana na mahitaji ya kituo hicho.
Alisema klabu hiyo imekuwa ikishirikiana nayo katika kusaidia mambo mbalimbali katika kituo hicho hivyo waendelee kuwasaidia watoto hao, ili baadae nao waje kuwa na maisha mazuri.
|
Rais wa Amani Lions Klabu ya Dar es Salaam, Dk. Hasan Husein akizungumza na watoto wa Kituo hicho baada ya kukabidhi msaada wa vyakula na mahitaji mengine yenye thamani sh. milioni 1.4. |
|
Mmoja wa Viongozi wa Amani Lions Klabu ya Dar es Salaam, Sharik Choughle akisalimiana na mlezi wa kituo hicho Bi. Hidaya Shukrani. |
|
Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Hisani cha kulea watoto yatima na wanaishi katika mazingira magumu, kilichopo Mbagala, Majimatitu, Dar es Salaam. |
|
Viongozi wa Amani Lions Klabu ya Dar es Salaam na watoto wa yatima na wanaishi katika mazingira magumu wa kituo cha Hisani wakiomba dua baada kutembelea na kutoa msaada. |
|
Mlezi wa Kituo cha Hisani Orphans Centre Trust, Hidaya Shukrani akishukuru baada ya kupokea msaada wa vyakula kutoka Amani Lions Klabu ya Dar es Salaam. |