Jumapili, 3 Agosti 2014

AMANI WOMEN GROUP (AWG) BYATOA MSAADA KWA WAGONJWA, OCEAN ROAD, DAR ES SALAAM.


Kikundi cha Wanawake, Amani Women Group, (AWG) wametoa misaada mbalimbali yenye thamani ya sh. milioni 1.5, kwa wagonjwa 250, katika Taasisi ya Saratani ya Ocean road.

Kikundi chenye wanachama 16, kilichopo Ukonga Mombasa, Dar es Salaam, kimetoa msaada huo kwa lengo la kuwafariji na kuwathamini wagonjwa hao kwani sehemu ya jamii.
Mwenyekiti wa Kikundi hicho Elizabeth Mshana Mbekenga alisema kazi mojawapo ya kukundi hicho ni kusaidiana katika masuala mbalimbali ya kiuchumi, jamii na Elimu.
Dk. Elizabeth alisema jamii inapaswa kutambua kuwa ngazi ya kusaidiana inaanzia katika jamii yenyewe kwa kutambua shida za wengine.

Hata hivyo aliotoa ushauri kwa wanawake nchini  kujiunga katika vikundi waweze kusadiana katika masuala ya kiuchumi, kijamii na kielimu na kujiletea maendeleo.Alisema wakiwa katika vikundi wataweza kukopeshana, kusaidiana na kupeana ushauri mbalimbali kwa ajili maendeleo yao.

Baadhi ya misaada iliyotolewa na Amani Wowen Group ikiwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dar es Salaam.

Viongozi na wanachama wa AWG, wakiwa katika picha ya pamoja Hospitalini hapo, baada ya kumaliza kazi ya kugawa misaada kwa wgonjwa.

Wakiandaa zawadi zao kwa ajili kurahisisha ugawaji ili kuhakikisha kila mgonjwa anapata.

Wanachama wa AWG, wakiwa ndani ya Hospitali hiyo kugawa zawadi zao kwa wagonjwa na kuwapa pole.


Mwenyekiti wa kikundi hicho, Dk. Elizabeth Mshana Mbekenga akimkabidhi mgonjwa zawadi pamoja na kumfariji katika wodi ya wanawake Ocean road.



Wakipongezana baada zoezi la kuwapa pole na kutoa zawadi kumalizika.






Hakuna maoni: