Jumatatu, 2 Juni 2014

MWILI MTOTO NASRA MVUNGI, WAPELEKWA MOROGORO KWA AJILI MAZISHI, KESHO.

Mwili wa mtoto Nasra Mvungi, leo umesafirishwa kuelekea Mkoani Morogoro kwa ajili ya Mazishi.
Mtoto Nasra alifanyiwa ukatili kwa kuweka ndani ya boksi kwa muda wa miaka minne na mama yake mdogo, hali iliyomsababishia umelema wa viungo.
Nasra alifikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akitokea katika Hospitali ya Morogoro anatarajiwa kuzikwa kesho ambapo ataagwa katika uwanja wa Jamuhuri.
Aidha, Ustawi wa Jamii ndio itakayoratibu mazishi ya mtoto huyo kutokana wao ndio waliokabidhiwa jukumu la mtoto tangia alipoibuliwa na wasamalia wema.
Hata hivyo baadhi ya ndugu wa mtoto huyo walikuwa katika eneo la Hospitali Muhimbili huku wakitaka kuuchukua mwili wa mtoto huyo kwa ajili mazishi.

R.I.P

Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mtoto Nasra  Mvungi, ambaye alihifadhiwa katika boksi kwa miaka minne, aliyefariki dunia juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),  alikokuwa akipatiwa matibabu.  Mwili huo ulisafirishwa jana  kwenda mkoani Morogoro kwa mazishi yatakayofanyika leo.

Baba mzazi wa Nasra, Rashid Mvungi akiwa nyuma ya gari akiangalia mwili mtoto wake ukupakiwa ndani ya gari aina ya Noah kwa ajili kusafirishwa kuelekea Morogoro.

Waombolezaji wakiwa na baba Mzazi wa marehemu Nasra  wakijadiliana kuhusu safari ya kuelekea Morogoro.

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

habari nzuri