Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utawala bora Geogre Mkuchika, amesema kumalizika kwa awamu ya kwanza ya mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi(OGP), kumetokea mabadiliko makubwa ya utoaji na upatikanaji wa taarifa Serikalini.
Alisema kujadiliwa kwa uwazi ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ni ishara kuonyesha nchi inavyoweka taarifa kunakopelekea uwajibikaji.
Mpango wa awamu ya pili utakaoanza mwaka wa fedha wa 2014/15 umepewa vipaumbele vinne vyenye lengo la kuboresha huduma za kijamii.
Aidha serikali katika kutekeleza mpango huo, mwishoni mwa mwaka huu inatarajia kutunga Sheria ya uhuru wa kupata habari ili upatikanaji wa habari uwe rahisi kwa wananchi.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Susan Mlawi amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za kimsingi za uendeshaji wa Serikali ikiwemo matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo.
Susan amesema Sheria hiyo itasaidia kuwepo kwa haki ya kimsingi ya upatikanaji wa taarifa na kuzuia urasimu unaojitokeza kudai haki ya kupata habari kwenye idara za kiserikali na binafsi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya OGP, Susan Mlawi akizungumza katika warsha hiyo kuhusu mpango huo ambao utakuwa manufaa kwa taifa. Kulia ni Kulia Katibu wa Kamati hiyo, Mathias Chitunchi. |
Waziri, Mkuchika akimakabidhi zawadi ya laptop mwanafunzi wa Msalato Sekondary, Sarah Kisusange aliyeshinda shindano la kuandika insha, yenye wazo bora kuhusu mpango huo. |
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Utawala Bora, George Mkuchika akiwa na Profesa Baregu wakijadiliana jambo, wakati wa warsha hiyo. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni