Mtoto Nasra alifanyiwa ukatili kwa kuweka ndani ya boksi kwa muda wa miaka minne na mama yake mdogo, hali iliyomsababishia umelema wa viungo.
Nasra alifikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akitokea katika Hospitali ya Morogoro anatarajiwa kuzikwa kesho ambapo ataagwa katika uwanja wa Jamuhuri.
Aidha, Ustawi wa Jamii ndio itakayoratibu mazishi ya mtoto huyo kutokana wao ndio waliokabidhiwa jukumu la mtoto tangia alipoibuliwa na wasamalia wema.
Hata hivyo baadhi ya ndugu wa mtoto huyo walikuwa katika eneo la Hospitali Muhimbili huku wakitaka kuuchukua mwili wa mtoto huyo kwa ajili mazishi.
R.I.P
Baba mzazi wa Nasra, Rashid Mvungi akiwa nyuma ya gari akiangalia mwili mtoto wake ukupakiwa ndani ya gari aina ya Noah kwa ajili kusafirishwa kuelekea Morogoro. |
Waombolezaji wakiwa na baba Mzazi wa marehemu Nasra wakijadiliana kuhusu safari ya kuelekea Morogoro. |
Maoni 1 :
habari nzuri
Chapisha Maoni