Ijumaa, 13 Juni 2014

MBUNGE WA KIBAHA VIJIJINI ATIMIZA AHADI ZAKE KWA WANANCH

Mbunge wa Hamoud Jumaa amevisaidia vikundi vya ujasaliamali katika jimb lake ikiwa ni sehemu ya kutekeleza ahadi alizozitoa katika kuleta maendeleo jimboni humo.
Jumaa alitoa msaada wenye thamani ya sh. milioni 25.

I.Mbunge wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa   akizungumza na Diwani wa Kata Bokomnemela Haruna   Issa na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo Winfrida Towegale   kuhusu ukarabati wa chumba cha darasa cha shule ya   msingi Bokomnemela.

Hamoud Jumaa akipima ukubwa wa dirisha.

Mbunge huyo akizungumza na kikundi cha VIKOBA cha Bokonmnela wakati alipofanya ziara ya kukagua jimbo lake na kutoa msaada kwa vikundi vya ujasiliamali.


Mbunge akimkabidhi hundi, Mwenyekiti wa kikundi cha Sisi kwa sisi VIKOBA kwa ajili kutunisha mfuko wa kikoba hicho.


Baadhi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika kitongoji cha Kaloleni, ambapo mbunge katika jimbo hilo alitoa hundi ya sh. 800,000, kusaidia sula la ada na sare za shule.

Mbunge huyo akikabidhi hundi hiyo mbele ya Diwani wa kata kata ya Janga, Fedilia Swai, Mwenyekiti wa Kamati ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu Shamte Matambala na Mwenyekiti wa Kitongoji hicho, Abdalah Kido.





Mbunge huyo wa Kibaha Vijijini akimkabidhi hundi ya sh. milioni 1.4, mwenyekiti wa Vijana Kata ya Kilangalanga kwa ajili maendeleo ikiwemo ufugaji nyuki, kilimo na korosho.

Hamoud akipata maelezo kutoka kwa wafugaji wa nyuki.



Mbunge huyo alikisaidia kikundi cha Kwala House Talent (KHT), hundi ya sh. milioni moja kwa ajili ya kuinua vipaji vya sanaa


Hakuna maoni: