|
Msemaji wa TFF, Boniface Wambura. |
Panoni FC na Geita Veterani, zimefanikiwa kutinga ligi Daraja la Kwanza baada ya kuongoza katika hatua ya makundi.
Panoni FC ilifanikiwa kuongoza kundi la Mbeya huku Mabingwa wa mkoa wa Mwanza Geita Vetelani wakiingia kupitia kituo cha Shinyanga.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface wambura alibainisha kuwa timu hizo zilifanikiwa kutinga ligi daraja la kwanza baada ya kuongoza kwenye vituo vyao.
Wambura alisema ligi ya mkoa ilitarajiwa kuhitimishwa leo katika kituo cha Morogoro ili kupata timu itakayoungana na Geita na Panoni kucheza ligi daraja la Kwanza msimu ujao.
"Timu za panoni Fc na Geita Vetelani zimefudhu kucheza ligi daraja la Kwanza baada ya kuongoza kwenye vituo vyao, ligi hiyo itahitimishwa leo kwenye kituo cha Morogoro," alisema wambura.
Alisema timu hizo zitashiriki Daraja la kwanza kutasaka nafasi ya kushiriki ligi kuu Tanzania bara.
MABONDIA KUPIMANA KUANZA KUPIMANA UBAVU KESHO
MICHUANO ya Kombe la Meya inatarajia kuanza kesho kwenye ukumbi wa Panandipanandi ambapo klabu kutoka Nairobi, Mombasa, Dar es Salaam, Arusha, Tanga na Morogoro zitashiriki.
Ofisa Habari wa Chama cha ngumi za Ridhaa mkoa wa Dar es Salaam, (DABA), Mwanvita Mtanda, alibaini hilo ambapo michuano hiyo inatarajia kuanza kesho hadi Juni 8 mwaka huu.
Mwanvita alisema michuano hiyo inalenga kutengeneza timu ya mkoa wa Dar es Salaam ambayo itashiriki michuano mbalimbali.
Alisema washindi watakaofanya vyema watapata kikombe, Medali na Vyeti vya ushiriki ambavyo vitatambuliwa na shirikisho la ngumi za kulipwa PST.
"Michuano ya kombe la meya itashrikisha timu kutoka nchini Kenya, itaanza saa 10.00, jioni hadi saa nne usiku,"alisema Mwanvita.
Aidha aliwaomba mashabiki wa masumbwi kujitokeza kwa wingi kushudia mpambano huo ambapo kiingilio ni sh.50,000.