BENKI ya Taifa ya Biashara imesema inampango wa kuwaongeza karani wa malipo , ili kupunguza foreni za wateja wanaochukulia fedha dirishani.
Hayo yalisemwa jana , Dar es Salaam na Meneja wa Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa benki hiyo Jane Dogan wakati wa maadhimisho ya siku ya huduma kwa wateja, iliyofanyika katika tawi la Sokoine.
Alisema wahudumu watakaoongenzwa tayari wako katika mafunzo ambapo mpango utakapokamilika utapunguza foreni kwani kwa sasa kumuhudumia wateja mmoja inachukua muda wa dakika 5 hadi 10.
Hata hivyo alisema benki hiyo katika kuboresha huduma zao wanatoa huduma ya kupokea na kutuma fedha kwa kutumia simu ya mkononi na katika mtandao wa intaneti.
Naye Mkurugenzi wa Benki hiyo Mizinga Melu alisema kuwa wanaathamanini wateja wao na ndio maana wanaendelea kuwahudumia kwa umahiri.
Alisema ni wajibu wao kutoa huduma ndio maana siku hiyo ya huduma kwa wateja wameamua kuwa wafanyakazi wote wajumuike pamoja katika kuwahudumia wateja wao.
“Tuko hapa wafanyakazi wote kuwasikiliza wateja wetu kuwahudumia tofauti na siku nyingine ambazo huwa tunakuwa ofisini ,” alisema Mizinga
Mkurugenzi wa benki ya NBC Mizinga Melu akizungumza na baadhi ya wateja katika benki hiyo wakati wa maadhimishohayo. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni