Jumamosi, 2 Novemba 2013

Manispaa ya Temeke na changamoto uzowaji taka.

HALMASHAURI ya Manispaa ya Temeke imesema haina uwezo wa fedha za kutoshereza kwa ajili ya uzowaji takataka zinazoongezeka kutokana na ongezeko la idadi ya watu na shughuli za uzalishaji katika manspaa hiyo.

Manispaa hiyo inakadiriwa kuzarisha wastani wa tani 1138, za takataka kwa siku, ambazo huzalishwa katika maeneo ya makazi ya watu na sehemu za kufanyia biashara.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, jana, katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Afisa Afya wa Mazingira wa manispaa hiyo Ernest Mamuya alisema kiasi cha taka kilichoshindwa kuondolewa ni kutokana na upungufu wa vitendea kazi.

Alisema kiasi hicho cha taka ambazo hazija zolewa ni wastani tani 599.5, ambazo ni sawa na 52, zinazodharishwa kwa siku katika maeneo mbalimbali.

Mamuya alisema vitendea kazi vinavyohitajika vian gharama kubwa na kupelekea manispaa hiyo kukosa fedha za kununulia, ndio maana taka nyingi zimeshindwa kuondolewa kwa wakati.

Afisa huyo alisema vifaa vinavyohitajika ili kukidhi mahitaji ya uzowaji taka ni magari sita ya kubebea makasha, makasha 60 ya kuhifadhia na kusafirishia taka, magari 10 kwa ajili ya kushindilia, mashine nne za kufagilia barabara, tela 26, trakta nne na malori 64 ya kubebea taka.

“Bajeti ya miradi ya maendeleo inayopangwa hutekelezwa kwa asilimia ndogo kutokana na fedha zake kutowasilishwa mapema kutoka serikali kuu, hivyo uchangia kucheleshwa uzowaji wa taka”, alisema.

Mamuya alisema matatizo mengine yanayosababishwa mlundikano wa taka ni kutokana na wananchi kushindwa kuchangia gharama za uzowaji, hivyo kuiongezea Halmashauri hiyo mzigo wa kugharamia na kusababisha kukwama kwa utekelezaji wa shughuli nyingine za kijamii.

Hakuna maoni: