Ijumaa, 28 Agosti 2015

Serikali ya Tanzania imetiliana saini makubaliano ya kuingia nchini kwa waangalizi/wasimamizi wa Uchaguzi mkuu kutoka nchi za Ulaya.


Shirika la Afya Dunian (WHO), limetoa msaada wa Dawa za kutakasa mazingira na kutibu maji ili kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu katika mkoa wa Dar es Salaam.

Wakazi wa Dar es Salaam, wametakiwa kuhakikisha wanazingatia kanuni za usafi ili kudhiti kuenea kwa ugonja wa Kipindupindu, ambapo umekuwa ukienea sehemu nyingi jijini humo.

Pia ugonjwa huo umueikumba mkoa wa Pwani ambapo hadi sasa wagonjwa saba wamekuwa wakipatiwa matibabu. Kati ya hao mmoja ameripotiwa kufariki dunia.

MATUKIO KATIKA PICHA

Mafanikio ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), ambapo limekuwa likitoa mafunzo ya stadi za kazi, Elimu ya Ujasiliamali, Kilimo, ufugaji.

Pia, Jeshi hilo likifundisha maadili kwa vijana ambao waliomaliza kidato cha sita kwa mujibu wa sheria.

Hizo ni baadhi ya shughuli zinazofanywa na jeshi hilo katika kambi ya Ruvu, wakati waandishi wa habari walipofanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali pamoja na huduma zinazotolewa.

Jeshi hilo limekuwa kwa karibu likishirikiana na wananchi hususan wakazi wa eneo jirani na kambi kwa kuwauzi vitu mbalimbali kwa gharama nafuu.

Jumapili, 17 Agosti 2014

LIONS CLUBS TANZANIA YAFANYA SEMINA YA SURUA NA RUBELLA.

Lions Clubs Tanzania in measles and Rubella Campaign is a successful drive to immunise the future of every developing country.
In Tanzania we have over 21, millions children under the age of 15 years ready for immunisation.
The campaign to sensitise all Tanzanias will commence from 1 to 6 September , while the immunisation programmes will take place from 24 to 27, september at over 13, 700 health centres in the whole country.
Lions Clubs Tanzania fraternity will mobilise its over 450, members to keenly participate and create awareness through various means from houses to schools in order that no child is left without the precious lifesaving vaccine.

Mratibu wa kampeni ya chanjo ya ugonjwa wa surua na rubella, Abdul Majeed, akiewaelezea wajumbe wa semina ya kupambana na magonjwa hayo, Dar es Salaam, jana.

Wajumbe wa semina wakisikiliza hotuba kutoka kwa Mratibu wa kampeni ya chanjo ya ugonjwa wa surua na rubella, Abdul Majeed.

Wajumbe kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania walihudhuria semina hiyo.

Wajumbe wakimsikiliza Meneja wa Mpango wa Taifa Chanjo, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Dafrossa Lyimo akitoa hutuba yake wakati wa semina hiyo.

Meneja  Mpango wa Taifa Chanjo, Wizara ya Afya na  Ustawi wa jamii, Dk. Dafrossa Lyimo, akieelezea wajumbe katika semina ya chanjo ya rubella na surua katika kupambana na magonjwa hayo, Dar es Salaam

Mratibu wa kampeni ya chanjo ya ugonjwa wa surua na rubella, Abdul Majeed, akizungumza na vyombo vya habari, Dar es Salaam.

Alhamisi, 7 Agosti 2014

NYUMBA NNE ZINAZODAIWA ZA MCHUNGAJI RWAKATALE ZIMEVUNJWA NA SERIKALI.

Nyumba hizo zilizoko maeneo ya Mbezi beach, Dar es Salaa, zilibomolewa na serikali kupitia Wizara ya Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Sabubu ya kubomolewa kwa nyumba hizo ni kujengwa katika kiwanja cha mjane aliyetambulika kwa jina la Janeth, ambako imeelezwa kuna kesi mahakamani baada ya kudaiwa Mchungaji Rwakatale amevamia katika kiwanja hicho.Licha Mahakama kutoa agizo la kutofanyika kwa kiu chocote katika kiwana hicho lakini imeelezwa kuwa Mchugaji Rwakatale  alikaidi amri hiyo na kuendelea na ujenzi.

Kijiko kikiendelea na zoezi la uvunjaji wa nyumba hizo.



Muonekano wa numba hio kabla ya kuvunjwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Mjane Janeth anayedaiwa kuwa ni mmiliki halali wa kiwanja hicho ambacho Mchungaji na Mbunge wa Viti maalum, Getrude Rwakatale amejenga.

Mlinzi aliyekuwa akilinda numba hizo akiangalia uvunjaji huo.


Jumapili, 3 Agosti 2014

AMANI WOMEN GROUP (AWG) BYATOA MSAADA KWA WAGONJWA, OCEAN ROAD, DAR ES SALAAM.


Kikundi cha Wanawake, Amani Women Group, (AWG) wametoa misaada mbalimbali yenye thamani ya sh. milioni 1.5, kwa wagonjwa 250, katika Taasisi ya Saratani ya Ocean road.

Kikundi chenye wanachama 16, kilichopo Ukonga Mombasa, Dar es Salaam, kimetoa msaada huo kwa lengo la kuwafariji na kuwathamini wagonjwa hao kwani sehemu ya jamii.
Mwenyekiti wa Kikundi hicho Elizabeth Mshana Mbekenga alisema kazi mojawapo ya kukundi hicho ni kusaidiana katika masuala mbalimbali ya kiuchumi, jamii na Elimu.
Dk. Elizabeth alisema jamii inapaswa kutambua kuwa ngazi ya kusaidiana inaanzia katika jamii yenyewe kwa kutambua shida za wengine.

Hata hivyo aliotoa ushauri kwa wanawake nchini  kujiunga katika vikundi waweze kusadiana katika masuala ya kiuchumi, kijamii na kielimu na kujiletea maendeleo.Alisema wakiwa katika vikundi wataweza kukopeshana, kusaidiana na kupeana ushauri mbalimbali kwa ajili maendeleo yao.

Baadhi ya misaada iliyotolewa na Amani Wowen Group ikiwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dar es Salaam.

Viongozi na wanachama wa AWG, wakiwa katika picha ya pamoja Hospitalini hapo, baada ya kumaliza kazi ya kugawa misaada kwa wgonjwa.

Wakiandaa zawadi zao kwa ajili kurahisisha ugawaji ili kuhakikisha kila mgonjwa anapata.

Wanachama wa AWG, wakiwa ndani ya Hospitali hiyo kugawa zawadi zao kwa wagonjwa na kuwapa pole.


Mwenyekiti wa kikundi hicho, Dk. Elizabeth Mshana Mbekenga akimkabidhi mgonjwa zawadi pamoja na kumfariji katika wodi ya wanawake Ocean road.



Wakipongezana baada zoezi la kuwapa pole na kutoa zawadi kumalizika.






Ijumaa, 1 Agosti 2014

HATIMAYE MFADHILI WA VITENDO VYA UGAIDI AFIKISHWA MAKAMANI.

                                                                     BREAKING NEWS!..

  Sheikh Farid Hadi Ahmed, ambaye anadaiwa kufadhili vitendo vya kigaidi nchini amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisitu, Dar es Salaam.



Mtuhumiwa Sheikh Farid akiwa chini ya ulinzi wa polisi, mahakamani hapo akipelekwa kwenye kizimba kwa ajili ya
kujibu mashtaka yanayomkabili ya kudaiwa kufadhili vitendo vya kigaidi.

Akiwa na mtuhumiwa mwenzake mahakamani hapo, wakitoka baada ya kila mmoja kusomewa mashtaka yanayomkabili.