Jumanne, 13 Mei 2014

MISRI YATOA VIFAA TIBA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI KUBORESHA HALI YA AFYA NCHINI.





Serikali Misri imepatia msaada wa vifaa tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), kwa ajili ya kuboresha huduma za Urolojia hospitalini hapo.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya sh. milioni 405,000,000, vilitolewa na Balozi wa Misri Nchini Hossam Mharam ambapo alimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo Dk. Marina Njelekela.

Huduma za Urolojia katika hospitali ya Taifa Muhimbili zilianzishwa mwaka 2008, chini ya Idara ya upasuaji  kwa lengo kuboresha huduma kwa wananchi.

Kitengo cha Urolojia hutoa huduma kwa wagonjwa wa uvimbe wa tezi dume (BPH), kuziba kwa njia ya mkojo kutokana na kovu (Urethra Stricture), saratani ya kibofu (Bladder Cancer), saratani ya tezi dume (Prostate Cancer) na mawe kwenye kibofu (Kidney Stone).

Akishikuru kwa niaba ya serikali, Mkurugenzi wa (MNH), Dk. Marina alisema vifaa tiba hivyo vimekuja wakati muafaka ambapo serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inatekeleza mkakati wake wa kuboresha huduma za afya

BALOZI wa Misri Nchini Tanzania, Hossam Moharam akimkabidhi vifaa tiba, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Marina Njelekela, wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam, jana.Katikati ni Daktari Bingwa Mshauri wa Urolojia Dk. Galal Ibrahim.





.

MCHAKATO WA KUCHUKUA FOMU ZA UONGOZI SIMBA NI MOTO, AVEVA NA WAMBURA WAWAPAGAWISHA MASHABIKI.

Mgombea nafasi ya rais katika klabu ya simba Michael Wambura akisindikizwa na wafuasi wake kwenda kuchukua fomu za kuomba ridha ya kuchagulia, Makao Makuu ya klabu hiyo, Msimbazi, Dar es Salaam.

Evansi Aveva akisindikizwa na Mzee Hassan Dalali kurudisha fomu ya kuwania nafasi ya urasi wa klabi ya simba, Makao Makuu ya klabu hiyo, Msimbazi, Dar es Salaam.


Wafuasi wa Aveva wakiwa klabuni hapo wakishangili mgombea wao kurudisha fomu za kuomba ridha ya kuchaguliwa.


Homa ya Dengue

Homa ya DENGUE husababishwa na virusi wanaoitwa DENGUE VIRUS kutoka familia ya FLAVIVIRIDAE. Wapo virusi wa aina tano katika familia hii na wote kwa pamoja au aina moja moja husababisha homa hii ya Dengue waingiapo mwilini kwa mwanadamu.

Virusi hawa husambazwa na mbu jike anayejulikana kitaalamu kwa jina la AEDES AEGYPTI. Kwa kumuangalia utamtambua mbu huyu kwani mwili wake unamadoa meupe kama anavyoonekana kwenye picha.

Inakadiliwa kiasi cha watu milioni 100 duniani kote huambukizwa homa ya Dengue kila mwaka na hasa maeneo ya Tropical ndio yanayoathirika zaidi.

kama nilivyokwisha eleza virusi wa homa ya dengue wanasambazwa na mbu anayejulikana kwa jina la aedes ambaye tayari anavirusi vya ugonjwa huu. Mbu huambukizwa virusi baada ya kumuuma mtu ambaye damu yake inavirusi vya ugonjwa wa dengue.
Ugonjwa wa dengue hauambukizwi kwa kugusana na mgonjwa au kula pamoja na mgonjwa.

DALILI ZA HOMA YA DENGU
Kawaida dalili huanza kuonekana siku ya 4 hadi sita baada ya maambukizi na hudumu kwa siku 10.
Dalili hizo ni pamoja na;
1.Homa kali ya ghafla.
2.Maumivu makali ya kichwa.
3.Maumivu nyuma ya macho.
4.Maumivu makali ya misuli na viungio (joints).
5.Kichefuchefu na kutapika.
6.kupata vipele ambavyo hutokea siku 3 hadi 4 baada ya       homa kuanza.
7.Kutokwa damu puani, katika fizi za meno na sehemu zenye jeraha.

Wakati fulani lakini mara chache sana homa hufikia hatua ya hatari ambapo mgonjwa anapatwa na homa kali sana, Tezi na njia za damu mwilini zinaharibika, anatokwa na damu kwa wingi puani na katika fizi za meno pia Maini huvimba na mfumo wa hewa unashindwa kufanya kazi. Homa ikizidi sana mgonjwa hutokwa na damu nyingi sana hupatwa na mshituko (shock) na hatimaye kifo.Hali hii kitaalamu inaitwa Dengue Shock Syndrome (DSS) au Dengue Hemorrhagic Fever (DHF).
Watu wenye mfumo zaifu wa kinga ya mwili na wale ambao waliwahi kuugua homa ya dengue na kupona wanauwezekano mkubwa zaidi wa kupatwa na Dengue Hemorrhagic Fever.

UTAMBUZI
Daktari ataweza kutambua kama mgonjwa anahoma ya dengue kwa kumpima damu na kuangalia kama anavirusi wanaoleta homa ya Dengue.

MATIBABU
Hakuna dawa sahihi inayotibu homa ya Dengue. Unachoweza kufanya ni kunywa dawa ya kutuliza maumivu isiyokua na aspirini(usinywe aspirini) kwasababu aspirini itachochea kutokwa na damu.
Kunywa juisi na maji kwa wingi..wahi hospitali kaonane na daktali pia pata muda wa kutosha wa kupumzika.

KINGA
Hakuna kinga ya kuzuia homa ya Dengue. Njia pekee kwa sasa ni kujikinga usiumwe na mbu anae eneza virusi vya ugonjwa wa Dengue. Vaa nguo ndefu, tumia chandarua, tumia dawa za kufukuza na kuua mbu, hakikisha katika nyumba yako mbu hawaingii ndani rekebisha milango na madirisha kwa kuwekea nyavu. Safisha mazingira yanayokuzunguka nyumbani kwako na hata unapofanyia kazi zako zinazokuingizia kipato, Fukia madimbwi na mashimo yenye maji kudhuia mbu wasizaliane na sehemu yoyote unapohifadhi maji hakikisha yanafunikwa na pia yasikae muda mrefu kabla ya kubadilishwa.
Kwakutunza mazingira yetu na kudhibiti mbu tutaweza kuzuia ugonjwa huu na magonjwa mengine yanayosambazwa na mbu kuenea.

ZINGATIA
Uonapo dalili yoyote kati zilizotajwa nenda hospitali kamuone daktari haraka.
MAJI yaliotwama ni chanzo cha mazalio ya mbu ambao wanaweza kueneza homa dengue.

Jumapili, 11 Mei 2014

CCM, IMEONGEZA WANACHAMA ZAIDI YA 500, AKIWEMO KATIBU WA CHADEMA WA TAWI PUGU STESHENI.MM

Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM, Wliaya ya Ilala, Tambwe Mbalima akikabidhi kadi za CCM, kwa mmoja wa wanachama wapya waliojiunga katika tawi la Pugu.

Mbalima akifungua shina la CCM, katika eneo la Pugu Stesheni. Kulia ni Mwenyekiti wa Tawi la Upgu Stesheni Fadhili Mgohamwelu.

Aliyekuwa Katibu wa CHADEMA, tawi la Pugu Bondeni Khadija Rajabu akivishwa furana ya CCN, baada ya kujiunga na chama hicho jana.


Khadija Rajabu akionyesha kadi yake ya CCM, baada ya kujiunga na chama hicho.

Wanachama wa CCM, wakiwa katika mkutano wa hadhara maeneo ya Pugu Stesheni.

MGOMBEA WA URAIS WA KLABU YA SIMBA EVANS AVEVA AKICHUKA FOMU.






WAKONGWE WA MADRID KUJA NCHINI MWEZI AGOST MWAKA HUU.






Real Madrid ya Hispania inatarajia kuja nchini mwezi Agost, mwaka huu kwa ajili ya mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania.

Jana, Mkurugenzi wa Makampuni ya TSN, Farough Baghoza na Nahodha wa klabu hiyo Ruben De la Red, walisaini mkataba wa ujio wa timu hiyo inawahusisha wachezaji waliowahi kuwika duniani na klabu hiyo.

Jumla ya wachezaji 25, wakongwe ambao waliowahi kuitumikia klabu hiyo kubwa Dunia wataambatana na wachezaji ambao wanaitumikia klabu hiyo hadi sasa.

Azungumzia ujio wa timu hiyo Mwakilishi wa TSN, Dennis Seboa alisema ujio wa wachezaji hao wakongwe watasaidia kuinua hali ya mchezo wa soka hapa nchini.

Sebo alisema wakongwe hao watapata nafasi ya kutembelea mbuga za wanyama kwa ajili kuitangaza utalii wa Tanzania, nchini Hispania ambapo aliyekuwa nahodha wa timu hiyo Fernando Hierro atapanda mlima Kilimanjaro ambapo televisheni ya Real madrid itaonyesha tukio hilo maja kwa moja.

Naye Nahodha wa timu hiyo ya wakongwe Ruben De la Red alisema wanatambua kuwa nchi ya Tanzania ina mashabiki wengi wanaopenda soka ambapo anaamini mechi hiyo itakuwa kali.

Aidha, alitoa angalizo kwa timu ya Tanzania kuwa wao bado wanafanya mazoezi kila siku na wako vizuri kiuchezaji hivyo timu ya vijana ya watanzania wafanye mazoezi ya kutosha.









Nahodha wa klabu ya wakongwe wa Real Madrid Ruben de la Red akizungumza na waandishi wa habari jana, Dar es Salaam, baada ya kutiliana saini na Makampuni ya TSN. Kushoto ni Mchezaji wa Klabu hiyo aliyewahi kuwika Rayo Gacial.


Rais wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF), Jamali Malinzi akikabiziwa jezi ya Madrid na Nahodha wa Ruben de la Red 
Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa akikabidhiwa jezi ya madrid.

WIKI YA UMOJA WA NCHI ZA ULAYA ILIVYOADHIMISHWA, DAR ES SALAAM, LEO.

Waziri wa Fya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid na Balozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya wakipingua mikono wakati wa maandamano ya kuelekea katika ufukwe wa bahari ya Hindi kwa ajili ya kufanya usafi wakati maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Nchi za Ulaya.

Washiriki wa maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Nchi za Ulaya wakifanya usafi katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Dar es Salaam.

Meya wa Manispaa ya Ilala Jery silaa akiwa na baadhi ya washiriki.

Wapanda baiskeri wakiwa katika maandamano ya amani wakati wa maadhimisho hayo.