Jumanne, 15 Julai 2014

MBRAZIL MWINGINE ATUA YANGA...

Genilson Santana Santos.
Mshambulaji kutoka nchini Brazil ametua katika Mkao Makuu ya klabu hiyo iloko mitaa ya Twiga na Jangwani kwa ajili kujiunga na klabu hiyo ambayo imepanga kuwa ya kimataifa.
 Santos, alitua katika ardhi ya Tanzania akitokea kwao saa 8.15, mchana ambapo alipokewa na viongozi mbalimbali wa klabu hiyo huku akilakiwa na wanachama wa yanga, ambapo alipelekwa moja kwa moja hadi klabuni hapo.
 Huyo ni mchezaji wa pili kutia katika klabu hiyo ambapo wakwanza Kiungo mshambuliaji,  Marcel Ferreira Coutinho.


Genilson Santana Santos, akiwasili katika Makao Mkauu ya Klabu ya Yanga kwa ajili ya kuingia kandarasi ya kuitumikia klabu hiyo.

Nimekuja kuwashika

Genilson Santana Santos.

Akisaini kitabu cha wageni klabuni hapo.

Afisa Habari wa Klabu ya Yanga baraka Kizuguto, akimkaribisha Santos, klabuni hapo.


Akiwasalimia baadhi ya wanachama na mashabiki wa Yanga.


Binda akizumtambulisha Santos baada kukanyaga katika klabuni hapo.


Wanachama na Mashabiki wa klabu ya Yanga wakiwa klabuni hapo kumwangalia Santos.


Jumamosi, 12 Julai 2014

SHARI K MWENYEKITI MPYA SHINA LA CCM, PAMBA ROAD, DAR ES SALAAM.

Mwenyeki wa mpya wa shina la  Wakeleketwa CCM, Pamba road, Sharik Choughule amesema atahakikisha chama hicho kinashinda chaguzi za serikali za mtaa na uchaguzi wa mkuu wa 2015.
Choughule alisema hayo juzi baada ya kuchaguliwa mwenyekiti mpya wa shina hilo katika uchaguzi uliofanyka katika ukumbi wa Karemjee, Dar es Salaam.
 Alisema kazi iliko mbele yake ni kuhakikisha kukiletea chama  maendeleo pamoja kuendeleza umoja uliko ndani ya shina hilo liloko katikati ya jiji la Dar es Salaam, maeneo ya Posta.
"Siwezi kuongea maneno mengi ila vitendo vyangu vitaonekana kwa kuiletea CCM, maendeleo na tawi shina letu, suala la msingi ni kushirikiana na wanachama wenzangu, kwani nina uzowefu wa uongozi kutokana na kuwa Kamanda wa Vijana Kata ya Kivukoni", alisema Choughule.

Sharik akwa na mpinzani wake kabla ya uchaguzi ndani ya ukumbi wa Karemjee, Dar es Salaam.


Wagombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Shina la CCM, Pamba road wakiwa mbele ya wapiga kura kabla ya kila mmoja kuomba kura.

Mwenyekiti  mpya wa Shina la Pamba Road Sharik Choughule akiwa mwenye furaha baada ya kumalizika kwa kuhesabiwa kura.

Wanachama wakipiga kura katika uchaguzi huo.
Akitangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa tawi hilo.

Akipongezwa na mpinzani wake aliyechuana naye katika uchaguzi uliomuweka madarakani Shariki, ambaye pia ni Kamanda wa Vijana, CCM, Kata ya Kivukoni.

Akikabidhiwa kiti rasmi na mwenyekiti wa uchaguzi, kulia ni Katibu wa shina.

Mwenyekiti mpya akinyanyuliwa juu juu 





Akisalimia wanachama akiwa makao Makuu ya Shina hilo la Pamba road, maeneo ya Posta, Dar es Salaam.

Mgombea aliyejitoa katika hatua za mwisho akipiga kura yake.








Jumatano, 9 Julai 2014

MAJADILIANO KUHUSU UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.

Mkutani uliofanyika jijini Dar es Salaam, Viongozi wa vyama vya walichangia mjadala kuhusu namna ya kuboresha daftari hili lilotarajiwa kuanza mwezi septemba mwaka huu, nchi nzima.
Katika mkutano huo vyama vya upinzani viliwakilishwa na viongozi wao akiweo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Wilbrod Slaa, Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu. Vyama vingine vilivyokuwa katika mkutano huo ni pamoja na Sauti ya Umma (SAU), CCK.
Mfumo mpya unaojulikana Biomettric Vote Registration (BVR), uliotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),  ambayo mwenyekiti wake ni Jaji Mstaafu Damian Lubuva.


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana akizungumza na vyombo vya habari wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa CUF, akielezea jambo kwa waandishi wa habari kuhusu mfumo huo mpya wa kuboresha daftari hilo.

Kushoto ni Tundu Lissu, Slaa na Lipumba wakiteta jambo kuhusu mfumo huo mpya wa kuliboresha daftari hilo la wapiga kura utakaoanza Septemba mwaka huu.

Dk. Slaa akitoa ufafanuzi kuhusu mfumo huo kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Lubuva.

Kinana akifuatilia kwa makini maakaratasi yenye taarifa kuhusu mkutano huo ambao ulikuwa unaelekeza namna ya mfumo huo wa BIOMATRIC VOTE REGISTRATION unaweza kufanyakazi.

Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini.

Kinana akizungumza jambo na Mwenyekiti wa UDP, John Cheo kwenye  mkutano wa viongozi wa vyama vya siasa kuhusu kujadili uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ulioandaliwa na Tume ya Taifa Uchaguzi(NEC), Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana akisalimiana na Katibu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa.

Mashine maalum itakayotumika kutengenezea vitambulisho vya kupigia kura, inajulikana BIOMATRIC VOTE REGISTRATION (BVR).

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (Mtaafu), Damian Lubuva akieleza kuhusu uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura kwa kutumia mfumo mpya Biometric Vote Regstration (BVR).




Jumatatu, 7 Julai 2014

KAMERA YETU MTAANI.

Tazama matukio ya kuvutia katika picha na uone uharisia wa maisha ya Watanzania.

Bidhaa zikishushwa katika soko la Buguruni, kunakopelekea kufurika kwa bidhaa sokoni hapo.

Barabara ya Kisutu, Dar es Salaam, ikiwa imeharibika kutokana na mvua zilizokuwa zinanyesha mwezi uliopita kunasababisha usumbufu kwa wapita njia.

Wajumbe wa kikao cha Jumuia ya Wazai kata ya Upanga Magharibi wakiwa nje ya ofisi ya Kata hiyo, baada ya ukumbi waliotakiwa kufanya kikao hicho kufungwa.

Ukosefu wa viwanda vidogo vidogo na kusindika matunda kunapelekea hasara ya matunda kuharibika. Machungwa yaliokosa wateja yakiwa yametelekezwa sokoni hapo.

Wateja wakinunua mihogo katika soko la Buguruni kwa ajili kutengenezea futari wakati wa kipindi hiki cha mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Ijumaa, 4 Julai 2014

MAXIMO ALIPOFANYA ZIARA KWENYE KLABU YAKE MPYA.

Kocha Mkuu wa Yanga amefanya ziara maalum ya kukagua uwanja, vyumba vya wachezaji katika klab yake ya Yanga ambapo ameomba kukarabatiwa kwa uwanja wa kaunda kwa ajili ya kufanyia mazoezi pamoja kuweka kiyoyozi katika ofisi atakayotumia klabuni hap.
Maximo aliongozana a viongozi wa klabu hiyo akiwemo Mwenyekiti Yussuf Manji, katib Mkuu Beno Njovu na msemaji klabu hiyo Baraka Kizuguto.

Maximo akielekeza jambo kuhusu jengo la klab yake mya ya Yanga.


Akitoa ushauri kuhusu ujenzi wa uwanja wa Kaunda kwa ajili ya kufanyia mazoezi.

Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji akielezea kuhusu mikakati ya klabu hiyo kwa Maximo.


Wakijadaliana kuhusu mikakati ya uwanja.


Wanachama wa Yanga wakiwa klabuni hapo kufuatilia mwenendo wa klabu yao.