Ijumaa, 28 Agosti 2015

Serikali ya Tanzania imetiliana saini makubaliano ya kuingia nchini kwa waangalizi/wasimamizi wa Uchaguzi mkuu kutoka nchi za Ulaya.


Shirika la Afya Dunian (WHO), limetoa msaada wa Dawa za kutakasa mazingira na kutibu maji ili kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu katika mkoa wa Dar es Salaam.

Wakazi wa Dar es Salaam, wametakiwa kuhakikisha wanazingatia kanuni za usafi ili kudhiti kuenea kwa ugonja wa Kipindupindu, ambapo umekuwa ukienea sehemu nyingi jijini humo.

Pia ugonjwa huo umueikumba mkoa wa Pwani ambapo hadi sasa wagonjwa saba wamekuwa wakipatiwa matibabu. Kati ya hao mmoja ameripotiwa kufariki dunia.

MATUKIO KATIKA PICHA

Mafanikio ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), ambapo limekuwa likitoa mafunzo ya stadi za kazi, Elimu ya Ujasiliamali, Kilimo, ufugaji.

Pia, Jeshi hilo likifundisha maadili kwa vijana ambao waliomaliza kidato cha sita kwa mujibu wa sheria.

Hizo ni baadhi ya shughuli zinazofanywa na jeshi hilo katika kambi ya Ruvu, wakati waandishi wa habari walipofanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali pamoja na huduma zinazotolewa.

Jeshi hilo limekuwa kwa karibu likishirikiana na wananchi hususan wakazi wa eneo jirani na kambi kwa kuwauzi vitu mbalimbali kwa gharama nafuu.